title : Jukwaa la kidigitali la Bizfundi lazinduliwa jijini Dar
kiungo : Jukwaa la kidigitali la Bizfundi lazinduliwa jijini Dar
Jukwaa la kidigitali la Bizfundi lazinduliwa jijini Dar
Naibu mkuu program ya Engine na kiongozi wa kitengo cha Mitaji na Ustawishaji, Scott Bennett (katikati) akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa Mradi jukwaa la kidigitali la Bizfundi kwa ajili ya kutoa usaidizi kwa wajasiliamali na wafanyabiashara ndogondogo kwa kuwaunganisha na wakufunzi na wataalamu wa masuala ya biashara kutambua haki zao. Pembeni kushoto ni mratibu wa ushirikiano wa taasisi hiyo, Immaculate Mwaungulu na kushoto ni Canisius Mwita.
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
Mradi wa kuwezesha ukuaji kupitia uwekezaji wa biashara (Engine) chini ya ufadhili wa shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), leo imezindua jukwaa la kidigitali la Bizfundi kwa ajili ya kutoa usaidizi kwa wajasiliamali na wafanyabiashara ndogondogo kwa kuwaunganisha na wakufunzi na wataalamu wa masuala ya biashara kutambua haki zao.
Jukwaa hilo lina lengo la kuongeza uwekezaji wa sekta binafsi na hatimaye kufanikisha kuwa na ukuaji wa uchumi ambao ni shirikishi na wenye wigo mpana kwenye mikoa ya Sagcotya Mbeya, Iringa, Morogoro na Zanzibar.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo jijini Dar es Salaam, Naibu mkuu program ya Engine na kiongozi wa kitengo cha Mitaji na Ustawishaji, Scott Bennett, amesema, Bizfundi itakuwa ni nyenzo ya kuzikutanisha biashara ndogondogo na za kati pamoja na wataalamu wa kutoa ushauri wa biashara na kutambua soko lao na kusaidiwa kuboresha utendaji na kukuza biashara zao.
“Jukwaa hilo la kidigitali ambalo linapatikana pia kwenye mtandao, litawawezesha wafanyabiashara ndogo ndogo kupata taarifa, usaidizi na mitaji inayohitajika wakati wa kutoa huduma za ushauri wa biashara na mashirika ya kifedha pia yataweza kunufaika na mtandao mkubwa zaidi wa wateja kwani mpaka sasa, jukwaa lina wamiliki wa bishara na watoa huduma za ushauri wapatao 200 waliojisajili,ammesema Bennet.
Amesema mpaka sasa Bizfundi imesajili wamiliki wa biashara zaidi ya 130,idadi ambayo inatarajiwa kupanda kutokana na muingiliano kati ya biashara ndogondogo na watoa huduma za ushauri wa biasharana kuongeza , kwa sasa Engine inashughulikia uundwaji wa huduma ya kuwaandaa wakopaji kitu kitakachosaidia wafanyabiashara ndogo ndogo kupata mikopo kwa shughuli zao.
Naye,mkuu wa kitengo hicho, Goodluck Mosha, amesema, jukwaa la Bizfundi litaleta ustawi na uwezo wa soko endelevu kwa watoa huduma za ushauri wa biashara kwa kuhakikisha wafanyabiashara ndogo ndogo na zile za kati zinaweza kupata kwa urahisi usaidizi wa kuimarisha biasharazao.
Hivyo makala Jukwaa la kidigitali la Bizfundi lazinduliwa jijini Dar
yaani makala yote Jukwaa la kidigitali la Bizfundi lazinduliwa jijini Dar Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Jukwaa la kidigitali la Bizfundi lazinduliwa jijini Dar mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/jukwaa-la-kidigitali-la-bizfundi.html
0 Response to "Jukwaa la kidigitali la Bizfundi lazinduliwa jijini Dar"
Post a Comment