title : Jela miaka kumi kwa kukutwa na silaha pamoja na risasi
kiungo : Jela miaka kumi kwa kukutwa na silaha pamoja na risasi
Jela miaka kumi kwa kukutwa na silaha pamoja na risasi
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Novemba 28/2017 imemuhuku mfanyabiashara Gairo Mtozoma (43), kutumikia kifungo cha miaka 10 jela baada ya kupatikana na hatia kukutwa na silaha pamoja na risasi.
Mshtakiwa Gairo ambaye pia ni mkazi wa Magomeni Kagera amehukumiwa kifungo hicho na Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa.
Akisoma hukumu hiyo, hakimu Mwambapa amesema, upande wa mashitaka ulileta mashahidi watano kwa ajili ya kuthibitisha mashitaka hayo na kwamba baada ya kusikiliza ushahidi huo mahakama ilimuona mshitakiwa kuwa na kesi ya kujibu na kujitetea mwenyewe.
Amesema kuwa katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi, mashitaka ya kwanza ya kupatikana na silaha, mshitakiwa huyo atatakiwa kutumikia kifungo cha miaka mitano jela na katika mashitaka ya pili atatumikia kifungo cha miaka mitano.
Kabla ya kutolewa kwa adhabu, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa iwe fundisho kwa wengine.
Katika kesi ya msingi, inadaiwa Agosti 11,2016 maeneo ya Magomeni Kagera wilayani Kinondoni, Mshtakiwa Gairo alikutwa na bastola moja aina ya Browing yenye kumbukumbu namba 90002 iliyosajiliwa kwa namba TZCAR-A222683 bila kuwa na leseni.
Pia inadaiwa Agosti 11,2016 maeneo ya Magomeni Kagera wilayani Kinondoni alikutwa na risasi sita bila kuwa na leseni.
Hivyo makala Jela miaka kumi kwa kukutwa na silaha pamoja na risasi
yaani makala yote Jela miaka kumi kwa kukutwa na silaha pamoja na risasi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Jela miaka kumi kwa kukutwa na silaha pamoja na risasi mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/jela-miaka-kumi-kwa-kukutwa-na-silaha.html
0 Response to "Jela miaka kumi kwa kukutwa na silaha pamoja na risasi"
Post a Comment