title : INDIA KUIKOPESHA TANZANIA DOLA MILIONI 500 KUJENGA MIRADI YA MAJI KATIKA MIJI 17 NCHINI
kiungo : INDIA KUIKOPESHA TANZANIA DOLA MILIONI 500 KUJENGA MIRADI YA MAJI KATIKA MIJI 17 NCHINI
INDIA KUIKOPESHA TANZANIA DOLA MILIONI 500 KUJENGA MIRADI YA MAJI KATIKA MIJI 17 NCHINI
Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam
Serikali ya India imeahidi kutoa mkopo nafuu wa Dola za Marekani milioni 500 kwa ajili ya kutekeleza mradi mkubwa wa maji katika miji 17 nchini kupitia Benki ya Exim ya nchini humo.
Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa India hapa nchini Bw. Sandeep Arya.Dkt. Mpango alieleza kuwa mradi huo umelenga kumtua ndoo mama kichwani na kwamba mkopo huo utakapo patikana utasaidia kutatua kero kubwa ya maji inayoikabili jamii hivyo kuchochea kwa kasi ukuaji wa uchumi.
“Tuko katika mazungumzo ya kukamilisha upatikanaji wa mkopo huo ikiwemo kuangalia namna ya kushughulikia madai ya Benki ya Exim ambayo inataka hata kampuni itakayotekeleza mradi huo isamehewe kodi zote zikiwemo zinazopaswa kulipwa na wafanyakazi wake” alieleza Dkt. Mpango
Alibainisha kuwa licha ya kwamba jambo hilo ni gumu kisheria lakini kutokana na umuhimu wa suala hilo la maji, Serikali italipatia ufumbuzi hivi karibuni ili mradi huo uweze kuanza mara moja.Dkt. Mpango alitambua mchango mkubwa wa Serikali ya India katika kutatua changamoto ya maji kwa watanzania ambapo amesema kuwa inchi hiyo inatatekeleza mradi mkubwa wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga hadi Tabora.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) wa pili kulia akielezea kuhusu uwekezaji wenye kuongeza thamani ya mazao ya kilimo ambao ni fursa kwa nchi hiyo, wakati wa Mkutano na Balozi wa India nchini Tanzania Bw. Sandeep Arya (wa pili kulia), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akiagana na Balozi wa India nchini Tanzania Bw. Sandeep Arya, baada ya kumalizika kwa mkutano kati yao Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa nne kulia), Balozi wa India nchini Tanzania Bw. Sandeep Arya, Maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Ubalozi wa India wakiwa katika picha ya pamoja, baada ya kumalizika kwa mkutano ulioangazia Uwekezaji na biashara, Jijini Dar es Salaam.Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango
Hivyo makala INDIA KUIKOPESHA TANZANIA DOLA MILIONI 500 KUJENGA MIRADI YA MAJI KATIKA MIJI 17 NCHINI
yaani makala yote INDIA KUIKOPESHA TANZANIA DOLA MILIONI 500 KUJENGA MIRADI YA MAJI KATIKA MIJI 17 NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala INDIA KUIKOPESHA TANZANIA DOLA MILIONI 500 KUJENGA MIRADI YA MAJI KATIKA MIJI 17 NCHINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/india-kuikopesha-tanzania-dola-milioni.html
0 Response to "INDIA KUIKOPESHA TANZANIA DOLA MILIONI 500 KUJENGA MIRADI YA MAJI KATIKA MIJI 17 NCHINI"
Post a Comment