title : DK. SHIKA USIKU WA 900 ITAPENDEZA NDANI YA DAR LIVE MBAGALA.
kiungo : DK. SHIKA USIKU WA 900 ITAPENDEZA NDANI YA DAR LIVE MBAGALA.
DK. SHIKA USIKU WA 900 ITAPENDEZA NDANI YA DAR LIVE MBAGALA.
Mwambawahabari
Meneja wa Dk Shika Catherine Kahabi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Na Maria Kaira,Mwambawahabari
Dk Shika anatarajia kukonga nyoyo za wakazi wa Dar es salaam siku ya Desemba 9 mwaka huu, katika hafla ya usiku wa 900 Itapendeza itakayofanyika katika ukumbi wa Dar live Mbagala ambapo ataongea na kuelezea historia yake alipotoka na alipo kwa sasa.
Dk.Luis Shika ni miongoni mwa watu waliopata umaarufu mkubwa kwa muda mfupi kutokana na kushinda mnada wa nyumba za Tajiri Lugumi na kuweza kumweka katika muonekano wa ubilionea.
Akizungumza na waandishi wa habari Leo Meneja wa Dk Shika Catherine Kahabi, amesema hafla hiyo iliyopewa jina ya Usiku wa 900 Itapendeza lengo likiwa ni kumtambulisha Dk Luis Shika kwa wakazi wa Dar es Salaam , waweze kumfahamu zaidi.
Amesema katika hafla hiyo kutakuwa na burudani mbalimbali wakiwemo wasanii wachekeshaji, akiwemo Mc pilipili, wasanii wa bongo fleva pamoja na bendi mbalimbali zitatumbuiza.
Aidha Mgeni rasmi.katika hafla hiyo anatarajiwa kuwa aliyekuwa waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi Lawrence Masha.
Hivyo makala DK. SHIKA USIKU WA 900 ITAPENDEZA NDANI YA DAR LIVE MBAGALA.
yaani makala yote DK. SHIKA USIKU WA 900 ITAPENDEZA NDANI YA DAR LIVE MBAGALA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DK. SHIKA USIKU WA 900 ITAPENDEZA NDANI YA DAR LIVE MBAGALA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/dk-shika-usiku-wa-900-itapendeza-ndani.html
0 Response to "DK. SHIKA USIKU WA 900 ITAPENDEZA NDANI YA DAR LIVE MBAGALA."
Post a Comment