title : WANANCHI WA HALMASHAURI YA MJI WA MADABA WAFURAHIA UJIO WA UMEME
kiungo : WANANCHI WA HALMASHAURI YA MJI WA MADABA WAFURAHIA UJIO WA UMEME
WANANCHI WA HALMASHAURI YA MJI WA MADABA WAFURAHIA UJIO WA UMEME
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MADABA.
WANANCHI wa Halmashauri ya mji wa Madaba, mkoani Ruvuma, wameipongeza serikali kwa kuwafikishia umeme kwenye eneo lao ambapo wamesema utabadilisha maisha yao.
Pongezi hizo zimetolewa Oktoba 11, 2017, kufuatia kukamilika kwa kazi ya kujenga njia ya kusafirisha umeme kwenye eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuweka mtandao wa nyaya (wiring), kwenye eneo hilo na kwenye nyumba za wananchi kazi iliyokwenda sambamba na ufungaji wa transofoma pozo.
Kwa sasa Serikali kupitia Shirika lake la Umeme, TANESCO inatekeleza mradi mkubwa wa umeme wa Makambako-Songea ambao unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovolti 220Kv Transmision Lines na usambazaji umeme vijijini (Rural electrification), katika vijiji vya mkoa wa Njombe na Ruvuma ikiwa ni pamoja na kujenga vituo viwili vipya vya kupoza umeme, huko Madaba na Songea na upanuzi wa kituo kingine mjini Makambako.
“Nimefurahi sana eneo letu kupata umeme, kwa muda mrefu sana tumekuwa tukitegemea umeme wa solar, sasa nina matumaini makubwa nimeona kazi zinavyoendelea hapa za kuweka nguzo za umeme, kutandaza nyaya majumbani na kuweka transofa, na tumeambiwa tukae mkao wa kula kwani umeem utawaka muda wowote kuanzia hivi sasa.” Anasema Rehema Maluwa, (pichani juu).
Nyumba zikiwa na madishi ya tv kwenye Halmashauri ya mji wa Madaba mkoani Ruvuma ambazo bila shaka kwa muda mrefu wamekuwa wakitumia fedha nyingi kutokana na matumizi ya jenereta kupata umeme lakini ujio wa umeme wa TANESCO utapunguza gharama za uendeshaji.
Maendeleo ya ujenzi wa msingi wa kufungia mashine kituo cha Madaba, ukiendelea Oktoba 11, 2017.
Maendeleo ya ujenzi wa msingi wa kufungia mashine kituo cha Madaba, ukiendelea Oktoba 11, 2017.
Mafundi wa TANESCO kwa kushirikiana na mkandarasi kutoka kampuni ya India ya Kalpataru, wakiwa kwenye eneo la ujenzi wa minara ya kupitisha laini za umeme wa 220kV huko Iboya, Njombe.
Mafundi wa TANESCO kwa kushirikiana na mkandarasi kutoka kampuni ya India ya Kalpataru, wakiwa kwenye eneo la ujenzi wa minara ya kupitisha laini za umeme wa 220kV huko Iboya, Njombe.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WANANCHI WA HALMASHAURI YA MJI WA MADABA WAFURAHIA UJIO WA UMEME
yaani makala yote WANANCHI WA HALMASHAURI YA MJI WA MADABA WAFURAHIA UJIO WA UMEME Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANANCHI WA HALMASHAURI YA MJI WA MADABA WAFURAHIA UJIO WA UMEME mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/wananchi-wa-halmashauri-ya-mji-wa.html
0 Response to "WANANCHI WA HALMASHAURI YA MJI WA MADABA WAFURAHIA UJIO WA UMEME"
Post a Comment