title : WANAFUNZI WAASWA KUNAWA MIKONO WATOKAPO MSALANI.
kiungo : WANAFUNZI WAASWA KUNAWA MIKONO WATOKAPO MSALANI.
WANAFUNZI WAASWA KUNAWA MIKONO WATOKAPO MSALANI.
SHULE mbili za manispaa ya Kinondoni zaadhimisha siku ya unawaji mikono ambayo hufanyika kila mwaka Oktoba 13 ikiwa na kaulimbiu ya mikono safi kwa manufaa ya sasa na ya baadae.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta amesema kuwa kila mtoto anatakiwa kunawa mikono kabla na baada ya kula pamoja na watokapo masalani ili kuepukana na maradhi ya kipindupindi na maradhi yaletwayo kwa kula uchafu.
Amesema kuwa siku hii ni muhimu hasa kwa watoto wanaokurupuka kumegeana vyakula au vitafunwa wawapo shuleni bila ya kunawa mikono yao na bila ya kujua ni nini madhara ya kula bila kunawa.
Pia amewaasa wanafunzi wa shule za msingi Mabibo pamoja na Mkwawa kunawa mikono mikono kila wanapotaka kula na baada ya kula pia marabaada ya kutoka maeneo ambayo wanashika uchafu.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Mabibo na shule ya msingi Mkwawa wakiwa katika siku ya kunawa mikono iliyoadhimishwa shuleni hapo kwaajili kuelewa manufaa ya kunawa mikono kabla ya kula, baada baada ya kula, na baada ya kutoka msalani kwaajili ya kujikinga na maradhi yanayoletwa na kuto kunawa mikono.
Mwanafunz wa chuo Kikuu cha Muhimbili Kerobe TEHSA akiwafundisha watoto jinsi ya kunawa mikono kwa kutumia kibuyu chirizi ambacho ni rahisi zaidi kuliko kuchota maji kwa kutumia kikombe ambayo ni kwaajili ya kunawa mikono kabla na baada ya kula na wakati watokapo msalani hii ikiwa ni siku ya unawaji Mikono iliyoambatana na kauli mbiu ya Mikono safi kwa manufaa ya sasa na yabaadae.
Hivyo makala WANAFUNZI WAASWA KUNAWA MIKONO WATOKAPO MSALANI.
yaani makala yote WANAFUNZI WAASWA KUNAWA MIKONO WATOKAPO MSALANI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANAFUNZI WAASWA KUNAWA MIKONO WATOKAPO MSALANI. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/wanafunzi-waaswa-kunawa-mikono-watokapo.html
0 Response to "WANAFUNZI WAASWA KUNAWA MIKONO WATOKAPO MSALANI."
Post a Comment