title : WANACHAMA WA MTANDAO WA KIJANI KIBICHI TANZANIA WAKAGUA SHAMBA LA UWEKEZAJI MKUBWA WA KILIMO CHA PAPAI RUAHA, IRINGA
kiungo : WANACHAMA WA MTANDAO WA KIJANI KIBICHI TANZANIA WAKAGUA SHAMBA LA UWEKEZAJI MKUBWA WA KILIMO CHA PAPAI RUAHA, IRINGA
WANACHAMA WA MTANDAO WA KIJANI KIBICHI TANZANIA WAKAGUA SHAMBA LA UWEKEZAJI MKUBWA WA KILIMO CHA PAPAI RUAHA, IRINGA
Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita) Mkakati wa Dkt. Kissui Stephen Kissui akielezea malengo ya ziara YA Wakulima wanachama wa mtandao huo walipowasili katika eneo la shamba hilo lililopo Ruaha- Kware, wilayani Kilolo, mkoani Iringa, patakapolimwa zao la kibiashara la Papai. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa mtandao huo, Adam Ngamange, Wa pili kushoto ni Afisa Mtendaji Kilimo na Mifugo wa Ruaha -Kware Wilaya ya Kilolo, John Mchopa, na Mwenyeji wa Shamba hilo na mkulima wa Ruaha, Amani Matinya.
Dk. Kissui amesema lengo ya ziara hiyo ni kuwaonesha Wakulima wanachama wa Mkikita mashamba wanayotarajia kuanza kulima kwa mkataba pia kuutangaza mtandao huo ili watu waanze kuwaza kijani na kila mtu arudi kwenye kilimo.
Alisema kama mtu hawezi kulima mwenyewe kuna wataalamu mbao watawekwa shambani kwa gharama nafuu ambao wataweza kuendeza mashamba hayo.
Pia, Dk. Kissui alisema wanatumia mbegu za kisasa zinazozalisha mara tatu zaidi na mbolea za Organic ambazo hazina madawa na haziharibu ardhi ili kuhakikisha vizazi na vizazi viweze kufurahia. Alisema pia Mkikita husaidia kutafuta masuala ya masoko duniani kabla ya kuanza kulima zao husika.
"Sisi tunaanza kutafuta masoko ya ndani na nje na baadaye tunawaaunganisha wakulima kwenye masoko" Alisema Kissui.
Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (MKIKITA) wakiwasili Ruaha -Kware Wilaya ya Kilolo, Mkoa wa Iringa wakati wa ziara ya kujionea shamba lenye ekari 3000 kwa ajili ya kuwekeza Kilimo cha PAPAI.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange akielezea miradi ya kuhamasisha kilimo na ufugaji kibiashara wakati wa ziara ya kutembela shamba kwa ajili ya kuwekeza kilimo cha PAPAI Ruaha -Kware Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa.
Hivyo makala WANACHAMA WA MTANDAO WA KIJANI KIBICHI TANZANIA WAKAGUA SHAMBA LA UWEKEZAJI MKUBWA WA KILIMO CHA PAPAI RUAHA, IRINGA
yaani makala yote WANACHAMA WA MTANDAO WA KIJANI KIBICHI TANZANIA WAKAGUA SHAMBA LA UWEKEZAJI MKUBWA WA KILIMO CHA PAPAI RUAHA, IRINGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANACHAMA WA MTANDAO WA KIJANI KIBICHI TANZANIA WAKAGUA SHAMBA LA UWEKEZAJI MKUBWA WA KILIMO CHA PAPAI RUAHA, IRINGA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/wanachama-wa-mtandao-wa-kijani-kibichi.html
0 Response to "WANACHAMA WA MTANDAO WA KIJANI KIBICHI TANZANIA WAKAGUA SHAMBA LA UWEKEZAJI MKUBWA WA KILIMO CHA PAPAI RUAHA, IRINGA"
Post a Comment