WAKULIMA WILAYANI BIHARAMULO WAIPONGEZA COSTECH KWA KUWAPELEKEA MBEGU BORA YA MIHOGO NA VIAZI LISHE

WAKULIMA WILAYANI BIHARAMULO WAIPONGEZA COSTECH KWA KUWAPELEKEA MBEGU BORA YA MIHOGO NA VIAZI LISHE - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAKULIMA WILAYANI BIHARAMULO WAIPONGEZA COSTECH KWA KUWAPELEKEA MBEGU BORA YA MIHOGO NA VIAZI LISHE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAKULIMA WILAYANI BIHARAMULO WAIPONGEZA COSTECH KWA KUWAPELEKEA MBEGU BORA YA MIHOGO NA VIAZI LISHE
kiungo : WAKULIMA WILAYANI BIHARAMULO WAIPONGEZA COSTECH KWA KUWAPELEKEA MBEGU BORA YA MIHOGO NA VIAZI LISHE

soma pia


WAKULIMA WILAYANI BIHARAMULO WAIPONGEZA COSTECH KWA KUWAPELEKEA MBEGU BORA YA MIHOGO NA VIAZI LISHE

Watafiti, Dk.Beatrice Lyimo (wa tano kushoto) na Bestina Daniel (wa pili kulia), kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),wakiwakabidhi mbegu bora ya mihogo Wanakikundi cha Chapakazi katika Kijiji cha Kalebezo wilayani Biharamulo mkoani Kagera jana, kwa ajili ya kuanzisha shamba darasa wakati wa uzinduzi wa shamba hilo wilayani humo. 

Na Dotto Mwaibale, Biharamulo Kagera.

WAKULIMA wilayani Biharamulo mkoani Kagera wameipongeza Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) pamoja na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB) kwa kuwapelekea mbegu bora ya migomba,mihogo na viazi lishe ambayo itapandwa katika mashamba darasa na kusambazwa kwa wakulima wengine katika wilaya hiyo.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwakilishi wa Ofisa Kilimo wa wilaya hiyo, Bruno Ngawagala wakati wa uzinduzi wa upandaji wa mbegu ya mhogo kwenye shamba darasa katika Kijiji Kalebezo wilayani humo.
Mwakilishi wa Ofisa Kilimo wa wilaya hiyo, Bruno Ngawagala (kulia), akizungumza na wakulima wakati wa uzinduzi wa upandaji wa mbegu ya mhogo kwenye shamba darasa katika Kijiji Kalebezo wilayani humo.

"Kwa niaba ya Ofisa Kilimo wa wilaya napenda kuishukuru COSTECH kwa kutuletea mbegu hizo katika wilaya yetu hasa baada ya kuona changamoto tuliyokuwa tukikabiliana nayo ya magonjwa ya mihogo kama batobato" alisema Ngawagala.

Ngawagala alisema msaada huo hautapotea bure kwani watahakikisha wanayahudumia vizuri mashamba darasa hayo likiwemo la mihogo lililopo katika Kijiji Kalebezo na lile la viazi lishe lililopo Kijiji cha Msenyi ambayo yamezinduliwa na kuhudhuriwa na wakulima kutoka vikundi vya Chapakazi katika Kijiji cha Kalebezo na Chapajembe cha Kijiji cha Msenyi vyote vya wilaya hiyo.

Mwenyekiti wa kikundi hicho cha Chapakazi, Thadeo Kibuka alisema mbegu hiyo waliyoletewa itakuwa mkombozi wao kwani kwa muda mrefu walikuwa na changamoto ya kupata mazao yenye magonjwa kutokana na kukosa mbegu bora na ukame.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Chapakazi, Thadeo Kibuka akizungumza katika uzinduzi huo.

"Tutahakikisha shamba ili tunalo lizindua leo hii kwa msaada wa COSTECH na OFAB linakuwa la mfano wa kuzalisha mbegu bora katika wilaya hii" alisema Kibuka.

Akizungumza kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH, Mtafiti Dk. Beatrice Lyimo alisema COSTECH kwa kushirikiana na OFAB wanaendesha mradi huo ili kuhakikisha kuhakikisha matokeo mazuri ya kazi za tafiti yanawafikia wakulima na kupata chakula cha kutosha.

Alisema COSTECH ndio mshauri mkubwa wa serikali katika masuala ya kilimo cha kitafiti hivyo wanakila sababu ya kuhakikisha tafiti zinazofanyika nchini zikiwafikia walengwa ili waweze kufanya vizuri katika kilimo.
Mtafiti kutoka COSTECH, Bestina Daniel, akizungumza.

Dk. Lyimo aliwataka wakulima hao kwa kushirikiana na maofisa ugani kuyatunza mashamba darasa hayo ili kupata mbegu nyingi za mazao hayo na kuzisambaza kwa wakulima wengine.



Hivyo makala WAKULIMA WILAYANI BIHARAMULO WAIPONGEZA COSTECH KWA KUWAPELEKEA MBEGU BORA YA MIHOGO NA VIAZI LISHE

yaani makala yote WAKULIMA WILAYANI BIHARAMULO WAIPONGEZA COSTECH KWA KUWAPELEKEA MBEGU BORA YA MIHOGO NA VIAZI LISHE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAKULIMA WILAYANI BIHARAMULO WAIPONGEZA COSTECH KWA KUWAPELEKEA MBEGU BORA YA MIHOGO NA VIAZI LISHE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/wakulima-wilayani-biharamulo-waipongeza.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAKULIMA WILAYANI BIHARAMULO WAIPONGEZA COSTECH KWA KUWAPELEKEA MBEGU BORA YA MIHOGO NA VIAZI LISHE"

Post a Comment