WAKULIMA WILAYA YA CHATO WAFURAHIA KUPATA MBEGU BORA KUTOKA COSTECH

WAKULIMA WILAYA YA CHATO WAFURAHIA KUPATA MBEGU BORA KUTOKA COSTECH - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAKULIMA WILAYA YA CHATO WAFURAHIA KUPATA MBEGU BORA KUTOKA COSTECH, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAKULIMA WILAYA YA CHATO WAFURAHIA KUPATA MBEGU BORA KUTOKA COSTECH
kiungo : WAKULIMA WILAYA YA CHATO WAFURAHIA KUPATA MBEGU BORA KUTOKA COSTECH

soma pia


WAKULIMA WILAYA YA CHATO WAFURAHIA KUPATA MBEGU BORA KUTOKA COSTECH

Na Dotto Mwaibale, Chato

WAKULIMA Wilaya Chato mkoani Geita wamefurahia mbegu bora ya mihogo, mahindi na viazi lishe waliopewa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ili kuanzisha mashamba darasa ya mbegu hizo na kuzisambaza kwa wakulima wengine katika maeneo mengine.

Wakizungumza wilayani hapa leo kwa nyakati tofauti wakati wa uzinduzi wa mashamba darasa ya mbegu hizo katika vijiji vya Kibehe, Ipandikilo, Kitongoji cha Kaseni, Kijiji cha Itale na Bukiliguru kilichopo Kata ya Bwanga walisema mbegu hizo walizokabidhiwa na COSTECH kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo ni mkombozi kwao.

Ofisa Kilimo wa Kata ya Kachwamba,  Hamisi  Matesi alisema Costech kuwapelekea wakulima mbegu hizo itawasaidia sana kupata chakula wananchi wa kata hiyo ziada watauza.

Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Ipandikilo, Clara Fidelis akizungumza kwa niaba ya wananchi wa kijiji hicho alisema wakulima walikuwa wakipata mavuno machache ya mahindi na mihogo kwa kuwa hawakuwa na mbegu bora hivyo baada ya kufunguliwa kwa shamba darasa la mbegu hizo katika maeneo yao wanategemea kupata mazao mengi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Chato, Mhandisi Joel Hari aliwataka wananchi hao kutambua kuwa mpango huo wa serikali ya awamu ya tano unawategemea sana wakulima katika kilimo hivyo fursa hiyo walioipata ya kupelekewa mbegu hizo wasiipoteze.

“Hakikisheni  mbegu hizi bora za mihogo mnazopewa mnazitunza  ili kutoa nafasi kwa wananchi wengi zaidi kujifunza mbinu bora za kilimo hiki kupitia shamba darasa hili ili kila mkazi wa Chato aweze kulima na kuzalisha kwa tija” alisema Mhandisi Hari.
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Viumbe Hai wa COSTECH, Dk.Bakari Msangi (kushoto), kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), akimkabidhi mbegu ya viazi lishe kwa ajili ya shamba darasa la Kijiji cha Kibehe, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Mhandisi Joel Hari wakati wa uzinduzi wa shamba hilo wilayani Chato leo. 
 Wanakikundi cha Umoja cha Kijiji cha Kibehe kilichopo Kata ya Kigongo wakiandaa shamba lao la mbegu.
 Wanakikundi cha Umoja cha Kijiji cha Kibehe kilichopo Kata ya Kigongo wakiwa kwenye uzinduzi wa shamba darasa la viazi lishe na mihogo.
 Mtafiti wa Mazao ya Mizizi wa Wilaya ya Chato, Monica Mulongo akizungumzia vitamini A inayopatikana kwenye viazi lishe ambayo ni muhimu kwa watoto.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala WAKULIMA WILAYA YA CHATO WAFURAHIA KUPATA MBEGU BORA KUTOKA COSTECH

yaani makala yote WAKULIMA WILAYA YA CHATO WAFURAHIA KUPATA MBEGU BORA KUTOKA COSTECH Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAKULIMA WILAYA YA CHATO WAFURAHIA KUPATA MBEGU BORA KUTOKA COSTECH mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/wakulima-wilaya-ya-chato-wafurahia.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAKULIMA WILAYA YA CHATO WAFURAHIA KUPATA MBEGU BORA KUTOKA COSTECH"

Post a Comment