WAFUGAJI NYUKI WATAKIWA KUANZISHA VIWANDA VIDOGO KUONGEZA THAMANI MAZAO YA NYUKI

WAFUGAJI NYUKI WATAKIWA KUANZISHA VIWANDA VIDOGO KUONGEZA THAMANI MAZAO YA NYUKI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAFUGAJI NYUKI WATAKIWA KUANZISHA VIWANDA VIDOGO KUONGEZA THAMANI MAZAO YA NYUKI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAFUGAJI NYUKI WATAKIWA KUANZISHA VIWANDA VIDOGO KUONGEZA THAMANI MAZAO YA NYUKI
kiungo : WAFUGAJI NYUKI WATAKIWA KUANZISHA VIWANDA VIDOGO KUONGEZA THAMANI MAZAO YA NYUKI

soma pia


WAFUGAJI NYUKI WATAKIWA KUANZISHA VIWANDA VIDOGO KUONGEZA THAMANI MAZAO YA NYUKI


Na Stella Kalinga, Simiyu

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng. Ramo Makani amesema Wafugaji Nyuki wanayo fursa kubwa ya kujikita katika uanzishwaji wa viwanda vidogo vidogo vya kuchakata, kufungasha na kuongeza thamani mazao ya nyuki na kutengeneza vipodozi kutokana na mazao ya nyuki.

Mhandisi Makani ameyasema hayo jana wakati alipozungumza na wafugaji wa nyuki na wananchi katika Maadhimisho ya Siku ya kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika katika Kijiji cha Isengwa Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, chini ya Kauli Mbiu “UFUGAJI NYUKI KIBIASHARA UNACHANGIA KATIKA UKUAJI WA VIWANDA”

Amesema Mazao ya Nyuki ni malighafi ya Viwanda mbalimbali vikiwemo viwanda vya vyakula vinavyotumia asali, viwanda vya dawa na vipodozi na viwanda vya utengenezaji vinavyotumia nta katika kuzalisha maturubai, dawa za kung’arisha viatu na bidhaa nyingine, hivyo wafugaji wanao wajibu wa kuongeza uzalishaji wa mazao ya nyuki na ujuzi wa kuyaweka katika ubora na kuyaongezea thamani.

Aidha, ametoa wito kwa wafugaji wa nyuki kuungana katika vikundi vyenye usajili ili waweze kuzalisha asali kwa wingi na yenye kufanana, kwa kuwa ikiwa watazalisha kila mmoja kwa utaratibu wake, asali hiyo haiwezi kuchanganywa na itakuwa na ubora na sifa tofauti, lakini ikiwa wataungana na kuzalisha asali nyingi kwa pamoja wakaipima kwa viwango vya ubora unaotakiwa wataweza kupata soko.

Sanjali na hilo amesema Serikali itahakikisha inawaunganisha wafugaji nyuki na walaji wa ndani na nje na akabainisha kuwa kwa miaka zaidi ya 11 imekuwa na ushirikiano na soko la Ulaya ambapo sampuli za asali kutoka maeneo mbalimbali zimepelekwa Ulaya na taarifa za maabara zinathibitisha kuwa asali ya Tanzania ni salama kwa afya ya mlaji.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng. Ramo Makani (Mb)(kulia)akitundika Mzinga katika Banda la Nyuki la Kikundi cha Wafugaji Nyuki cha Malela wakati wa Maadhimisho ya siku ya kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika jana katika Kijiji cha Isengwa Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng. Ramo Makani (Mb)akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Itilima(hawapo pichani ) wakati wa Maadhimisho ya siku ya kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika jana katika Kijiji cha Isengwa Wilayani humo katika Mkoa Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe.Benson Kilangi akizungumza na wananchi wa wilayani hiyo (hawapo pichani ) wakati wa Maadhimisho ya siku ya kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika jana katika Kijiji cha Isengwa Wilayani humo katika Mkoa Simiyu.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng. Ramo Makani(Mb) akizindua Manzuki (Shamba la Miti lenye Mizinga ya Nyuki) ya Kikundi cha Wafugaji nyuki cha Malela Wilayani Itilima wakati wa Maadhimisho ya siku ya kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika jana katika Kijiji cha Isengwa Wilayani humo katika Mkoa Simiyu.




Hivyo makala WAFUGAJI NYUKI WATAKIWA KUANZISHA VIWANDA VIDOGO KUONGEZA THAMANI MAZAO YA NYUKI

yaani makala yote WAFUGAJI NYUKI WATAKIWA KUANZISHA VIWANDA VIDOGO KUONGEZA THAMANI MAZAO YA NYUKI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAFUGAJI NYUKI WATAKIWA KUANZISHA VIWANDA VIDOGO KUONGEZA THAMANI MAZAO YA NYUKI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/wafugaji-nyuki-watakiwa-kuanzisha.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAFUGAJI NYUKI WATAKIWA KUANZISHA VIWANDA VIDOGO KUONGEZA THAMANI MAZAO YA NYUKI"

Post a Comment