WAANDISHI WA HABARI WASHAURIWA HABARI ZA VIJIJINI

WAANDISHI WA HABARI WASHAURIWA HABARI ZA VIJIJINI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAANDISHI WA HABARI WASHAURIWA HABARI ZA VIJIJINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAANDISHI WA HABARI WASHAURIWA HABARI ZA VIJIJINI
kiungo : WAANDISHI WA HABARI WASHAURIWA HABARI ZA VIJIJINI

soma pia


WAANDISHI WA HABARI WASHAURIWA HABARI ZA VIJIJINI


Na Pamela Mollel,Morogoro

Waandishi hapa nchini wameshauriwa kuongeza muamko katika kuandika na kutangaza habari za vijijini kwa kuwa asilimia 75 ya wananchi wa Tanzania wanaishi vijijini, ambako wanaendesha maisha yao kwa kufanya shughuli mbalimbali

Rai hiyo imetolewa leo Mkoani Morogoro na mwenzeshaji Joe Nakajumo katika mafunzo ya uandishi wa habari za vijijini iliyowakutanisha wanahabari kutoka mikoa mbalimbali iliyoratibiwa na umoja wa vilabu vya habari Tanazania (UTPC).

Nakajumo alisema kuwa waandishi wa habari wanajukumu kubwa la kuwa karibu na jamii ya vijijini kwa kutambua shughuli zao wanazozifanya na kuzifatilia kwa kuona mafanikio yao pamoja na kuibua kero zinazowakabili

“Asilimia 75 ya wananchi wanaishi vijijini wanaendesha maisha yao kwa kufanya shughuli za kilimo,ufugaji ,uvuvi,ujasiriamali hivyo ni muhimu sana  kuwapa kipaumbela wananchi hawa”alisema Nakajumo.Aidha alisema kuwa moja ya majukumu ya msingi ya mwandishi wa habari ni kusaidia na kushiriki katika ujenzi wa taifa hivyo anapaswa kuudhihirishia umma kwa watu wote nchini wanapaswa kupata habari

Kwa upande wake mshiriki wa semina hiyo Adam Juma alisema kuwa mafunzo haya yatasaidia kuibua changamoto vijijini ambako panaoneka kusaulika kwa huduma mbalimbali za kijamii.Pia aliwaomba waandaji wa semina hii UTPC kuendeleza mafunzo haya kwa waandishi wa habari ili kuweza kuwajengea uwezo wa kufanya kazi kwa kuzingatia misingi ya taaluma hiyo

Umoja wa vilabu vya habari Tanazania(UTPC)imekuwa ikiendelea kutoa mafunzo mbalimbali kwa waandishi wa habari lengo ikiwa kuwaongezea ujuzi wa kufanya kazi zao kwa kufata misingi ya taaluma .
Waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali wakiwa katika mafunzo ya uandishi wa habari za vijijini mkoani Morogoro ,Semina hiyo imeratibiwa na umoja wa vilabu vya habari Tanazania(UTPC).
Mwezeshaji wa semina Joe Nakajumo akifundisha katika mafunzo hayo leo Mkoani Morogoro.
Kushoto ni Noria Damian ,katikati Editha Carlo pamoja Happines Mtweve wakifatilia mafunzo hayo.
Kushoto ni mwakilishi kutoka Arusha Press club Pamela Mollel,katikati ni Adam Juma kutoka Mtwara Press Club wakifuatilia mafunzo hayo.



Hivyo makala WAANDISHI WA HABARI WASHAURIWA HABARI ZA VIJIJINI

yaani makala yote WAANDISHI WA HABARI WASHAURIWA HABARI ZA VIJIJINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAANDISHI WA HABARI WASHAURIWA HABARI ZA VIJIJINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/waandishi-wa-habari-washauriwa-habari.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAANDISHI WA HABARI WASHAURIWA HABARI ZA VIJIJINI"

Post a Comment