title : UWT MKOA WA MBEYA WATOA ELIMU YA AFYA YA UZAZI KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI
kiungo : UWT MKOA WA MBEYA WATOA ELIMU YA AFYA YA UZAZI KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI
UWT MKOA WA MBEYA WATOA ELIMU YA AFYA YA UZAZI KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI
Na Mwandishi wa Globu ya Jamii Mbeya
Umoja wa wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) wilaya ya Mbeya mjini imeendesha zoezi la kutoa elimu ya afya ya uzazi na Maendeleo kwa wanafunzi wa shule ya kutwa ya Mbeya .
Akizungumza na Globu ya Jamii Katibu wa UWT Mkoa wa Mbeya , Mary Mwenisongole amesema kuwa kwa kushirikiana na wataalam wa afya na Maendeleo ya jamii,leo tarehe wameshiriki kutoa elimu ya afya na kujitambua kwa watoto wa kike zaidi ya 500 shule ya sekondari ya kutwa Mbeya ikiwa ni sehemu ya maazimisho ya wiki ya miaka 39 ya jumuiya ya wanawake.
'' Sisi kama Jumuiya ya Wanawake wa chama kikongwe hapa nchini tumeona kuwa katika shamra shamra za miaka zaidi ya 38 ya Jumuiya yetu ndani ya chama ni vyema tukaanza kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa watoto wa kike waliopo mashuleni kwani wao ndio Viongozi wa UWT ya baadae" amesema .
Akishukuru kwa niaba ya ya Walimu mwalimu wa nidhamu Benson John aliishukuru jumuiya kwa jambo walilofanya na kuomba waendelee kwani tatizo la mimba ni kubwa na kwa mwaka huu 2017 kufikia mwezi wa 9 wanafunz 6 wameshindwa kuendelea na masomo yao kutokana na tatizo la ujauzito.
UWT mkoa wa Mbeya imewahakikishia walimu kuwa zoezi hili lita kuwa endelea na katibu UWT ameahidi kufika mara nyingi iwezekanavyo kupitia mpango wa sauti ya shangazi ambayo imepokelewa kwa shangwe, na wanafunzi wameahidi kutoa ushirikiano kwa SHANGAZI.
Katibu wa UWT mkoa wa Mbeya, Mary Mwenisongole akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kutwa ya Mbeya katika programu ya Ongea na Shangazi
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mbeya Mjini Mama Mtani akizungumza na na Wanafunzi wa kike wa Mbeya kutwa.
Hivyo makala UWT MKOA WA MBEYA WATOA ELIMU YA AFYA YA UZAZI KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI
yaani makala yote UWT MKOA WA MBEYA WATOA ELIMU YA AFYA YA UZAZI KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UWT MKOA WA MBEYA WATOA ELIMU YA AFYA YA UZAZI KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/uwt-mkoa-wa-mbeya-watoa-elimu-ya-afya.html
0 Response to "UWT MKOA WA MBEYA WATOA ELIMU YA AFYA YA UZAZI KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI"
Post a Comment