title : Tumieni Wataalam wa Utafiti katika Ujenzi-NHBRA
kiungo : Tumieni Wataalam wa Utafiti katika Ujenzi-NHBRA
Tumieni Wataalam wa Utafiti katika Ujenzi-NHBRA
Na. Paschal Dotto- MAELEZO.
Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) imewashauri wananchi kufuata maelekezo katika ujenzi wa nyumba za makazi na majengo mbalimbali ili kupata nyumba bora.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam Mhandisi Benedict Chila alisema kuwa kuna uhitaji mkubwa sana wa utafiti kwa nyumba za makazi kuhusu matumizi bora ya vifaa vya ujenzi kama matofali, kokoto pomoja na mchanga uliobora katika ujenzi.
“kuna uhitaji mkubwa wa tafiti ambazo zitawawezesha watanzania kupata makazi bora yenye kudumu, kwani katika vifaa na huduma zinazopatikana kwetu zinajikita zaidi katika usanifu majengo pamoja na matumizi ya vifaa, kwa hiyo tafiti hizi ni muhimu kwa wananchi wenye mahitaji ya makazi bora”,.alisema Mhandisi Chila.
Aidha Mhandisi Chila alisema kuwa katika kutambua uhitaji wa wananchi NHBRA imetoa mlango kwa jamiii kupata huduma bora kwa kufanya tafiti katika sanifu ya majengo na vifaa vya kutumia katika ujenzi ili kupata makazi bora.
Mmoja wa wafanyakazi katika Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) akitengeneza vigae vya kuezekea nyumba vilivyofanyiwa utafiti Jijini Dar es Salaam tayari kwa matumizi ya ujenzi wa nyumba.
Ukuta unaofanyiwa utafiti kwa ujenzi wa kutumia tofali mbichi kwa majengo makubwa na nyumba za makazi ulioko katika karakana ya Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) Jijini Dar es Salaam.
Mhandishi na fundi sanifu wa majengo Bw.Hussein Mataka akitoa maelezo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani ) kuhusu mashine ya kufyatua tofali iliyoko katika karakana la ofisi hizo Mwenge Jijini Dar es Salaam.
Mhandisi wa ofisi za Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) Bw. Benedict Chilla akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu huduma zinazotolewa na ofisi hiyo mapema wiki hii Jiji Dar es Salaam.
Mashine ya kupima ubora na kiwango cha udongo kwa ujenzi wa nyumba ambayo ni moja ya vifaa bora vinavyopatikana Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) kama inavyoonekana kwenye picha.Picha na Paschal Dotto-MAELEZO
Hivyo makala Tumieni Wataalam wa Utafiti katika Ujenzi-NHBRA
yaani makala yote Tumieni Wataalam wa Utafiti katika Ujenzi-NHBRA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Tumieni Wataalam wa Utafiti katika Ujenzi-NHBRA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/tumieni-wataalam-wa-utafiti-katika.html
0 Response to "Tumieni Wataalam wa Utafiti katika Ujenzi-NHBRA"
Post a Comment