title : Simba wamaliza kambi Zanzibar na kurejea Dar
kiungo : Simba wamaliza kambi Zanzibar na kurejea Dar
Simba wamaliza kambi Zanzibar na kurejea Dar
Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Kikosi cha Simba kimeondoka Visiwani Zanzibar leo saa 3 za asubuhi kwa Ndege na kurejea jijini Dar es Salaam kwa maandalizi ya mwisho ya mechi yao ya kesho ya ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Yanga kwenye uwanja wa Uhuru.
Akizungumza na Mtandao huu wakati waondoka hapa Zanzibar kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema akili yao yote ni kuifunga Yanga kesho kwenye uwanja wa Uhuru huku akiwataka Mashabiki wa Simba waendelee kuishangiria timu yao.
“Kambi ya Zanzibar ilikuwa nzuri sana naamini tumefikia malengo yetu, hapa tunaondoka na leo jioni Dar tutafanya mazoezi ya mwisho, nawaomba Mashabiki wa Simba wazidi kuishangiria timu yao”. Alisema Manara.
Simba walikuwa kambini mjini hapa tangu Jumatatu ya Oktoba 23 na leo Ijumaa Oktoba 27 wamerejea nyumbani Dar es salam kuwavaa Yanga.
Hivyo makala Simba wamaliza kambi Zanzibar na kurejea Dar
yaani makala yote Simba wamaliza kambi Zanzibar na kurejea Dar Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Simba wamaliza kambi Zanzibar na kurejea Dar mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/simba-wamaliza-kambi-zanzibar-na.html
0 Response to "Simba wamaliza kambi Zanzibar na kurejea Dar"
Post a Comment