title : SIDO WATOE MAFUNZO KWA WANAFUNZI WA VYUO ILI WAJIAJIRI: RC NCHIMBI.
kiungo : SIDO WATOE MAFUNZO KWA WANAFUNZI WA VYUO ILI WAJIAJIRI: RC NCHIMBI.
SIDO WATOE MAFUNZO KWA WANAFUNZI WA VYUO ILI WAJIAJIRI: RC NCHIMBI.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amelitaka shirika la Viwanda Vidogo vidogo (SIDO) kuandaa mafunzo ya ujasiriamali kwa wanafunzi wa vyuo mbali mbali mkoani hapa ili wakihitimu waweze kujiajiri
Dkt. Nchimbi ametoa wito huo wakati akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mikopo ya SIDO kwa wajasiriamali iliyofanyika kwenye viwanja vya SIDO ambapo amesema mafunzo hayo yatawajengea mazingira mazuri wahitimu kujiajiri.
Amesema Mkoa wa Singida una fursa nyingi za kujiajiri pamoja na kuwa na vijana wengi hasa walipo katika vyuo mbalimbali lakini hawawekezi katika fursa hizo kwa kutokujua au kukosa elimu ya kutosha juu ya ujasiriamali, na hata waliopo vyuoni wakihitimu wanasubiri kuajiriwa badala ya kujiajiri.
Dkt. Nchimbi amesema ili wananchi wakiwemo vijana waweze kuzitambua fursa hizo, SIDO Mkoa na wadau wengine wanapaswa kuongeza juhudi zaidi katika utoaji mafunzo ya ujasiriamali ambapo amewataka wajielekeze kwenye vyuo mbalimbali.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akitoa hundi ya Mkopo uliotolewa na SIDO kwa mjasiriamali Sarah Isaya kutoka Singida katika hafla fupi ya kukabidhi mikopo kwa wajasiriamali mbalimbali mkoani hapa.
Mkurugenzi Mtendaji SIDO Taifa Mhandisi Profesa Sylvester Mpanduji akitoa nasaha zake kwenye hafla ya utoaji wa hundi za mikopo kwa wajasiriamali mbalimbali mkoani Singida uliofanyika kwenye viwanja vya SIDO mjini hapa. Wa kwanza kushoto (aliyekaa) ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi.
Meneja wa SIDO Mkoa wa Singida Shoma Kibende akitoa taarifa ya Viwanda Vidogo vidogo na ujasiriamali Mkoa wa Singida kwenye hafla ya utoaji wa hundi za mikopo kwa wajasiriamali mbalimbali. Wa kwanza kushoto (waliokaa) ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi na Mkurugenzi Mtendaji SIDO Taifa Mhandisi Profesa Sylvester Mpanduji.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala SIDO WATOE MAFUNZO KWA WANAFUNZI WA VYUO ILI WAJIAJIRI: RC NCHIMBI.
yaani makala yote SIDO WATOE MAFUNZO KWA WANAFUNZI WA VYUO ILI WAJIAJIRI: RC NCHIMBI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SIDO WATOE MAFUNZO KWA WANAFUNZI WA VYUO ILI WAJIAJIRI: RC NCHIMBI. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/sido-watoe-mafunzo-kwa-wanafunzi-wa.html
0 Response to "SIDO WATOE MAFUNZO KWA WANAFUNZI WA VYUO ILI WAJIAJIRI: RC NCHIMBI."
Post a Comment