title : SERIKALI YAHITIMISHA ZOEZI LA UHAKIKI WA NGOs NCHINI
kiungo : SERIKALI YAHITIMISHA ZOEZI LA UHAKIKI WA NGOs NCHINI
SERIKALI YAHITIMISHA ZOEZI LA UHAKIKI WA NGOs NCHINI
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto imehitimisha zoezi la uhakiki kwa Mashirika Masiyo ya Kiserikali nchini ulioanza Mwezi Agosti mwaka 2017.
Akizungumza wakati wa kutoa taarifa kwa umma kuhusu kukamilisha zoezi hilo Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga amesema kuwa jukumu la Wizara ni kusajili na kuratibu shughuli za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa mujibu wa Sera ya kitaifa ya Mashirikka Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2001.
Ameongeza kuwa Serikali imeendelea kuimarisha uratibu wa mashirika yasiyo ya kiserikali nchini kwa kuimarisha mifumo ya uratibu kwa kushirikiana na Halmashauri zote nchini.Bibi Sihaba Nkinga ameyataka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kuzingatia Sheria, taratibu na kanuni zilizopo katika kuendesha kazi zao katika kuhudumia jamii.
“Tumekamilisha zoezi hili kwa kipindi tulichokiweka na ninawaomba wadau wetu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo katika utendaji wa shughuli zao la kila siku” alisema Bibi Sihaba.bibi Sihaba mefafanua kuwa Mashirika ambayo hayakuweza kuhakikiwa kwa sababu za msingi katika kipindi chote cha uhakiki, yanatakiwa kufika Ofisi ya Msajili wa NGOs ili kukamilisha zoezi hilo na mara baada ya tarehe hiyo muda wa uhakiki utasitishwa na mashirika hayo hayataruhusiwa kufanya kazi yoyote nchini kwa kushindwa kuzingatia taratibu.
Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga(kushoto) akizungumza na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na waandishi wa habari Mjini Morogoro wakati akihitimisha zoezi la uhakiki wa NGOs nchini ulioanza Mwezi Agosti Mwaka 2017 kulia ni Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Marcel Katemba.
Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Marcel Katemba akiwashukuru wadau wa mashirika yasiyo ya Kiserikali nchini kwa ushirikiano wao katika zoezi zima la uhakiki wa NGOs nchini kushoto ni Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga.
Baadhi ya watendaji wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wadau wa Mashirika Yasiyo ya kiserikali nchini wakimsikiliza Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga( hayupo pichani) wakati wa zoezi la kuhitimishwa kwa zoezi la uhakiki wa Mashirika Yasiyo ya kiserikali nchini.
Hivyo makala SERIKALI YAHITIMISHA ZOEZI LA UHAKIKI WA NGOs NCHINI
yaani makala yote SERIKALI YAHITIMISHA ZOEZI LA UHAKIKI WA NGOs NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAHITIMISHA ZOEZI LA UHAKIKI WA NGOs NCHINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/serikali-yahitimisha-zoezi-la-uhakiki.html
0 Response to "SERIKALI YAHITIMISHA ZOEZI LA UHAKIKI WA NGOs NCHINI"
Post a Comment