title : Puma Energy yaendeleza udhamini wake Rock City Marathon
kiungo : Puma Energy yaendeleza udhamini wake Rock City Marathon
Puma Energy yaendeleza udhamini wake Rock City Marathon
KAMPUNI ya mafuta ya Puma Energy leo imekabidhi hundi yenye thamani Tsh milioni 25 kwa waandaaji wa mbio za Rock City Marathon ikiwa ni mwendelezo wa kampuni hiyo kudhamini mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Octoba 29 mwaka huu, Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Akikabidhi hundi hiyo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo Bw Zenno Ngowi, Meneja Mkuu wa kampuni ya Puma Energy Bw Phillipe Corsaletti alisema udhamini huo unalenga kuunga mkono juhudi za serikali kuhamasisha michezo na utalii wa ndani hapa nchini.
“Michezo huleta uimara wa afya na uimara huo ndio umetufikisha Puma Energy hapa tulipo kimafanikio. Ni wazi ushiriki wa Puma kwenye mbio hizi utawajaza nishati ya nguvu na ubora washiriki wote’’ alisema.
Aliahidi kuwa kampuni yake itaendelea kushirikiana na waandaaji wa mbio hizo katika kuboresha zaidi mbio hizo kwa miaka ijayo huku akitoa wito kwa vijana wengi zaidi kutoka mikoa mbalimbali kujiandaa kwa ajili ya mbio hizo.
Akizungumza baada ya kupokea hundi hiyo, Ngowi alisema uwepo wa kampuni hiyo katika kufanisha Rock City Marathon utaongeza hadhi na ubora wa mbio hizo ili ziende sambamba na ubora wa huduma na bidhaa zinazoandaliwa na kampuni hiyo.
Naye, Mratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI), Bw. Bidan Lugoe alisema pamoja na medali washindi wa kwanza wa mbio za kilomita 42 kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh. Mil 4 kila mmoja, Sh mil 2/- kwa washindi wa pili na sh. Mil 1/- kwa washindi wa tatu.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Puma Energy Bw Phillipe Corsaletti (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh milioni 25 kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio za Rock City Marathon Bw Zenno Ngowi (wa tatu kushoto) ikiwa ni udhamini wa mbio hizo wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Wengine ni pamoja na Meneja Masoko wa Kampuni ya Puma Energy Bw Machumani Shebe (wa tatu kulia) na Mratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI), Bw. Bidan Lugoe (kulia)
Meneja Masoko wa Kampuni ya Puma Energy Bw Machumani Shebe (kushoto) akizungumza kwenye warsha hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio za Rock City Marathon Bw Zenno Ngowi (katikati) akizungumza kwenye warsha hiyo. Pamoja na mambo mengine Ngowi alisema uwepo wa kampuni ya Puma katika kufanisha Rock City Marathon utaongeza hadhi na ubora wa mbio hizo ili ziende sambamba na ubora wa huduma na bidhaa zinazoandaliwa na kampuni hiyo.
Mratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI), Bw. Bidan Lugoe akizungumza kuhusiana na maandalizi ya mbio hizo ambazo pamoja na medali washindi wa kwanza wa mbio za kilomita 42 kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh. Mil 4 kila mmoja, Sh mil 2/- kwa washindi wa pili na sh. Mil 1/- kwa washindi wa tatu.
Hivyo makala Puma Energy yaendeleza udhamini wake Rock City Marathon
yaani makala yote Puma Energy yaendeleza udhamini wake Rock City Marathon Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Puma Energy yaendeleza udhamini wake Rock City Marathon mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/puma-energy-yaendeleza-udhamini-wake.html
0 Response to "Puma Energy yaendeleza udhamini wake Rock City Marathon"
Post a Comment