Naibu Waziri Shonza:Vijana jiungeni na vikundi vya Mazoezi

Naibu Waziri Shonza:Vijana jiungeni na vikundi vya Mazoezi - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Naibu Waziri Shonza:Vijana jiungeni na vikundi vya Mazoezi, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Naibu Waziri Shonza:Vijana jiungeni na vikundi vya Mazoezi
kiungo : Naibu Waziri Shonza:Vijana jiungeni na vikundi vya Mazoezi

soma pia


Naibu Waziri Shonza:Vijana jiungeni na vikundi vya Mazoezi

Naibu Waziri wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (mwenye tisheti nyeupe katikati) akiwa katika mazoezi ya jogging na kikundi cha Kawe Jogging Social Club katika sherehe za miaka mitano ya kikundi hicho zilizofanyika leo jijini Dar es Salaam (aliyenyoosha kidole kushoto) ni Katibu wa Kawe Jogging Social Club Bw.Alhaj Seif Muhere.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (mwenye tisheti nyeupe katikati)akifanya mazoezi ya viungo na wanachama wa vikundi mbalimbali vya jogging mkoani Dar es Salaam katika sherehe za miaka mitano ya kikundi cha Kawe Jogging Social Club leo,(kushoto) Katibu wa Kawe Jogging Social Club Bw.Alhaj Seif Muhere na kulia ni Mwanachama wa Jogging Kawe Social Club Bi Felister Mwijage.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akizungumza na wanachama wa vikundi mbalimbali vya jogging Mkoani Dar es Salaam katika sherehe za maadhimisho ya miaka mitano ya kikundi cha Kawe Jogging Social Club zilizofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Na Anitha Jonas – WHUSM

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza ametoa wito kwa vijana kujiunga na vikundi vya mazoezi maarufu kama (Jogging Club) kwa ajili ya kuimarisha afya zao na kujikwamua kiuchumi.

Mheshimiwa Naibu Waziri ametoa wito huo katika sherehe za maadhimisho ya miaka mitano ya Kawe Jogging Social Club zilizofanyika leo jijini Dar es Salaam ambapo aliwapongeza wanachama wa Klabu hiyo kwa kuweza kudumu kwa muda wote huo.

“Napenda kuwapongeza kwa juhudi zenu pamoja na ubunifu mliyoutumia katika kujiongezea kipato kupitia klabu yenu kwa kuanzisha mgahawa ambao unawaongezea kipato na kukuza uchumi wenu kwa hakika mmekuwa ni mfano wa kuigwa,”Mhe. Shonza.

Akiendelea kuzungumza katika sherehe hizo Naibu Waziri huyo amewahakikishia wanaklabu hao ushirikiano pamoja na kushughulikia maombi yao ya kupatiwa mashine ya maximalipo.

Naye Mwenyekiti wa Kawe Jogging Social Club Bw. Abdul Risasi alimshukuru Naibu Waziri kwa kujumuika nao katika sherehe hiyo na kutoa ombi la kusaidiwa kupata mfadhili atakayeweza kuwasaidia kufanikisha ushiriki wao katika mashindano ya Kilimarathon yanayotarajia kufanyika Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.

“Tumekuwa tunashiriki katika mashindano ya Kilimanjaro Marathon kwa miaka minne mpaka sasa na Kawe Jogging Social Club imekuwa ndiyo kikundi pekee nchi nzima ambacho kimepata nafasi ya kuweza kushiriki mashindano hayo ambapo wanachama wake hukimbia mpaka kilometa 21,”alisema Bw.Risasi.

Pamoja na hayo Mwenyekiti huyo aliendelea kutoa wito kwa vijana kujiunga katika vikundi vya jogging kwani kupitia umoja huo wanaweza kujitengeneza fursa za kiuchumi na kujiongezea kipato badala ya kukaa vijiweni na kulalamikia hali ngumu ya maisha.

Kwa upande wa mmoja wa wanachama wa Msasani Jogging Club Bi Asha Said alitoa maoni yake na kusema jogging clubs ni nzuri kwani zinasaidia kupata marafiki pamoja na kuimarisha afya.


Hivyo makala Naibu Waziri Shonza:Vijana jiungeni na vikundi vya Mazoezi

yaani makala yote Naibu Waziri Shonza:Vijana jiungeni na vikundi vya Mazoezi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Naibu Waziri Shonza:Vijana jiungeni na vikundi vya Mazoezi mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/naibu-waziri-shonzavijana-jiungeni-na.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Naibu Waziri Shonza:Vijana jiungeni na vikundi vya Mazoezi"

Post a Comment