title : MKAZI WA CHATO GEITA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUCHAPISHA TAARIFA ZA UONGO MTANDAONI
kiungo : MKAZI WA CHATO GEITA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUCHAPISHA TAARIFA ZA UONGO MTANDAONI
MKAZI WA CHATO GEITA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUCHAPISHA TAARIFA ZA UONGO MTANDAONI
MKAZI wa Chato Geita, Obadia Frank (41), alipokua akingia katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaa leo kusomewa mashtaka yanayomkabili ya Kuchapisha taarifa ya uongo chato Geita.
MKAZI wa Chato Geita, Obadia Frank (41), akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Mara baada ya kusomewa mastaka yanayomkabiri jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
Na Karama Kenyunko Bloguya Jamii.
MKAZI wa Chato Geita, Obadia Frank (41), mapema leo amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni.
Akisomewa hati ya mashtaka na wakili wa serikali Leornad Challo amedai mshtakiwa huyo ambayeni wakala wa Baypot ametenda kosa hilo gosti 8 mwaka huu, katika Wilaya ya Chato mkoani Geita.
Mbele ya Hakimu Mkazi Wilbard Mashauri imedaiwa kuwa siku hiyo mshtakiwa Frank alichapisha taarifa kupitia ukurasa wake wa facebook inayosema,Taarifa kutoka kikao cha mazungumzo kati ya serikali na wawakilishi wa kampuni ya Acacia kuwa wanasheria wa upande wetu wanashindwa kutafsiri baadhi ya vifungu vya sheria hadi kufikia kuomba msaada kwa wanasheria wa Acacia sasa huoni hivi ni vituko mwizi anakusaidia sharia haahaa haha.
Mazungumzo bado yanaendelea lakini wanasheria wetu wamebanwa sana ukizingatia wale jamaa wanavielelezo vyote vya mikataba kiukweli tumuombe mungu maaa serikali ikitaka kkuvunja mkataba na Acacia gharama kubwa zitatuhusu lakini pia kuendekeza vyama itatugharimu sana baada ya Mh. Rais Magufuli angewashilikisha wakina mawakili wasomi waliokwiva wakili Tundu Lisu, wakili Kibatara na Fatma Karume kwenye mambo muhimu kama haya yeye kaleta uchama sasa itatugarimu// DitectaMagufulimustgo”
Imedaiwa mshtakiwa ametenda hayo huku akijua kuwa taarifa hizo ni uongo na zilikuwa na nia ya kuipotosha jamii
Hata hivyo mshtakiwa huyo anayetetewa na wakili Peter Kibatala, amekana kutenda kosa hilo na amerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza mashtari na kesi hiyo itatajwa Octoba 16 mwaka huu.
Mahakama imemtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wakuaminika ambao walitakuwa kuweka bondi ya milioni tano.
Hivyo makala MKAZI WA CHATO GEITA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUCHAPISHA TAARIFA ZA UONGO MTANDAONI
yaani makala yote MKAZI WA CHATO GEITA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUCHAPISHA TAARIFA ZA UONGO MTANDAONI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MKAZI WA CHATO GEITA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUCHAPISHA TAARIFA ZA UONGO MTANDAONI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/mkazi-wa-chato-geita-kizimbani-kwa.html
0 Response to "MKAZI WA CHATO GEITA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUCHAPISHA TAARIFA ZA UONGO MTANDAONI"
Post a Comment