title : Meli ya kifahari ya Mfalme wa Oman yawasili Dar es salaam kutokea Zanzibar
kiungo : Meli ya kifahari ya Mfalme wa Oman yawasili Dar es salaam kutokea Zanzibar
Meli ya kifahari ya Mfalme wa Oman yawasili Dar es salaam kutokea Zanzibar
Meli ya kifahari ya Mfalme wa Oman Mhe. Qaboos bin Said ‘Fulk Al Salamah’ iliyofika Zanzibar Oktoba 12, 2017, imeng’oa nanga leo mchana kuelekea Dar es Salaam kuendelea na safari yake ya kusambaza ujumbe wa ‘Amani na upendo’ duniani.
Taarifa kutoka ubalozi mdogo wa Oman zimeeleza kuwa, meli hiyo itakaa Dar es Salaam kwa siku nne kabla kuelekea Mombasa Kenya kwa madhumuni hayo hayo.
Akizungumza baada ya kuagana na ujumbe wa meli hiyo bandarini Zanzibar, Balozi Mdogo wa Oman Dk. Al Habsi, ameishukuru Serikali ya Mapinduzi Zanzbar chini ya Rais wake Dk. Ali Mohamed Shein na wananchi wote kwa mapokezi mazuri na ukarimu mkubwa waliouonesha kwa ndugu zao wa Oman.
Ameomba hali hiyo iendelee, akisema mahaba na ukarimu ndiyo mambo yanayowafungamanisha Wazanzibari na Waomani ambao kihistoria ni ndugu wa miaka mingi.
Meli ya Kifahari ya Mfalme Qaboos wa Oman FULK AL SALAMAH ikiingia katika Bandari ya Zanzibar ikitokea Oman ikiwa na Lengo la kuimarisha umoja Amani na Upendo,ikiongozwa na Waziri wa Mafuta na Gesi Dkt,Mohammed Bin Hamed Al Rumhi wa Serikali ya Oman.
Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idi wapili kushoto akisalimiana na Waziri wa Mafuta na Gesi wa Serikali ya Oman Dkt,Mohammed Bin Hamed Al Rumh mara baada ya kuwasili kwa Meli ya Kifahari ya Mfalme Qaboos wa Oman FULK AL SALAMAH wakiwa na ziara ya siku Nne kwa Lengo la kuimarisha umoja Amani na Upendo Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idi kulia akisalimiana na Mabaharia mara baada ya kuingia katika Meli ya Kifahari ya Mfalme Qaboos wa Oman FULK AL SALAMAH iliofika katika Bandari ya Zanzibar pamoja na Waziri wa Mafuta na Gesi wa Serikali ya Oman kwa Ziara ya Siku Nne ikiwa na lengo la kuimarisha umoja Amani na Upendo Zanzibar. PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.
Hivyo makala Meli ya kifahari ya Mfalme wa Oman yawasili Dar es salaam kutokea Zanzibar
yaani makala yote Meli ya kifahari ya Mfalme wa Oman yawasili Dar es salaam kutokea Zanzibar Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Meli ya kifahari ya Mfalme wa Oman yawasili Dar es salaam kutokea Zanzibar mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/meli-ya-kifahari-ya-mfalme-wa-oman.html
0 Response to "Meli ya kifahari ya Mfalme wa Oman yawasili Dar es salaam kutokea Zanzibar"
Post a Comment