Matukio : PSPF Yawazawadia Wafanyakazi wake kwenye kilele cha Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani

Matukio : PSPF Yawazawadia Wafanyakazi wake kwenye kilele cha Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Matukio : PSPF Yawazawadia Wafanyakazi wake kwenye kilele cha Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Matukio : PSPF Yawazawadia Wafanyakazi wake kwenye kilele cha Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani
kiungo : Matukio : PSPF Yawazawadia Wafanyakazi wake kwenye kilele cha Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani

soma pia


Matukio : PSPF Yawazawadia Wafanyakazi wake kwenye kilele cha Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani



NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, amewapongeza wafanyakazi wa Mfuko huo, kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuwatumikia wateja, (wanachama) wa Mfuko.
Bw. Mayingu ameyasema hayo wakati wa hafla fupi ya kuwatunuku tuzo na zawadi wafanyakazi waliofanya vizuri zaidi katika kipindi cha Wiki ya Huduma kwa Wateja, iliyoanza Oktoba 2 na kumalizika Oktoba 6, 2017.
Wiki hiyo ambayo huadhimishwa kila mwanzo wa wiki ya mwezi Oktoba kila mwaka, hulenga kuwakumbusha wafanyakazi wajibu wao wa kuwahudumia wateja kwa kuzingatia weledi wa utoaji huduma bora kwa mteja.
"Wakati nikiwa Iringa nimepokea pongezi nyingi za Wanachama wetu, wakiwapongeza nyinyi wafanyakazi kwa kuwahudumia vizuri, hongereni sana na niwaombe muendele kutoa huduma bora kwa wateja wetu kwani huo ndio wajibu wetu." Alisema Bw. Mayingu katika hafla hiyo iliyofanyika Oktoba 6, 2017 kwenye ukumbi wa makao makuu ya PSPF, Jubilee Tower jijini Dar es Salaam.
Bw. Mayingu aliwapongeza wafanyakazi wa Mfuko huo kote nchini, kwa kazi nzuri na kuwaeleza kuwa kitendo cha wafanyakazi na maafisa wa Mfuko huo kutoka maofisini na kuwafata wateja, (wanachama) majumbani kwao ili kuzungumza nao na kuwahudumia kimesifiwa sana.
"Kaimu Mkurugenzi Mkuu, alifuatana na baadhi yenu kwenda kule Kipunguni B. na kukutana na mwanachama wetu, Bw. Kassim Mafanya, ambaye alikipongeza kitedo kile na kusema hakutegemea maishani mwake yeye kama mstaafu angetembelewa nyumbani kwake na PSPF, hili ni jambo jema." Alibainisha Bw. Mayingu.
Wafanyakazi waliopata tuzo ni Elizabeth Shayo, kutoka kitengo cha Huduma Kwa Wateja, Makao Makuu, ambaye kupitia teknolojia, (mifumo), ni wateja wenyewe ndio waliompendekeza kutokana na maoni yaliyopokelewa lakini idadi ya watu aliowahudumia.
Mwingine ni Bi.Valley Malinga, Afisa kitengo cha simu (Call Centre), ambaye naye alitunukiwa tuzo na kupewa zawadi kutokana na kuhudumia idadi kubwa ya wateja bila kuchoka.
Tuzo hizo pia zimekwenda kwa walezi wa mikoa wa PSPF, kampuni mshirika ya Ardhi Plan Limited na pia makampuni washirika yaliyoshirikiana na PSPF kwenye wiki ya huduma kwa wateja, ambayo ni pamoja na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), Mabenki ya CRDB, NMB, TPB na Mwalimu Commercial Bank (MCB).

Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, akiwahutubia wafanyakazi na wadau wa Mfuko, wakati wa hafla ya kuwatunuku tuzo na kuwakabidhi zawadi wafanyakazi "waliochomoza" kwa utoaji huduma bora zaidi katika kipindi cha Wiki ya Huduma kwa Wateja, 2017, iliyofikia kilele Oktoba 6, 2017.

Bw. Mayingu akimkabidhi tuzo, Elizabeth Shayo.

Bw. Mayingu akimkabidhi tuzo, Bi.Valley Malinga

Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), Bi. Mwanjaa Sembe, (wapili kushoto), akiwa na maafisa waandamizi wa Mfuko huo.

Baadhi ya wafanyakzi wa PSPF

Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, akiwahutubia wafanyakazi na wadau wa Mfuko, wakati wa hafla ya kuwatunuku tuzo na kuwakabidhi zawadi wafanyakazi "waliochomoza" kwa utoaji huduma bora zaidi katika kipindi cha Wiki ya Huduma kwa Wateja, 2017, iliyofikia kilele Oktoba 6, 2017.


Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Neema Muro, akihutubia wakati wa hafla ya kuwatunuku wafanyakazi wa Mfuko huo mwshoni mwa Wiki ya Huduma kwa Wateja makao makuu ya Mfuko jijini Dar es Salaam Oktoba 6, 2017



Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Neema Muro, akihutubia wakati wa hafla ya kuwatunuku wafanyakazi wa Mfuko huo mwshoni mwa Wiki ya Huduma kwa Wateja makao makuu ya Mfuko jijini Dar es Salaam Oktoba 6, 2017



Meneja wa Huduma kwa Wateja, Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Laila Maghimbi, (kulia), na AfIsa Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. January Buretta, wakihakikisha kila kitu kinakuwa sawa kwenye hafla hiyo


Baadhi ya wadau wa PSPF waliohudhuria hafla hiyo


Sehemu ya wafanyakazi waliohudhuria hafla hiyo.



Sehemu ya wafanyakazi waliohudhuria hafla hiyo.



Sehemu ya wafanyakazi waliohudhuria hafla hiyo.


Baadhi ya wadau wa PSPF waliohudhuria hafla hiyo

Bw. Mayingu akimkabidhi tuzo Afisa Uendeshaji Mwandamizi wa PSPF Bw. Delphin Richard, (kushoto)

Bw. Mayingu akimpatia zawadi Afisa Mipango Miji wa kampuni mshirika na PSPF, Ardhi Plan Limited, Bi. Anna Lukindo.

Mkurugenzi Mkuu na viongozi wengine wa Mfuko wakiwa katika picha ya pamoja na watunukiwa wa tuzo

Picha ya pamoja na wadau


Hivyo makala Matukio : PSPF Yawazawadia Wafanyakazi wake kwenye kilele cha Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani

yaani makala yote Matukio : PSPF Yawazawadia Wafanyakazi wake kwenye kilele cha Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Matukio : PSPF Yawazawadia Wafanyakazi wake kwenye kilele cha Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/matukio-pspf-yawazawadia-wafanyakazi.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Matukio : PSPF Yawazawadia Wafanyakazi wake kwenye kilele cha Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani"

Post a Comment