title : MANJI AACHIWA HURU KWA KUKOSEKANA USHAHIDI WA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA
kiungo : MANJI AACHIWA HURU KWA KUKOSEKANA USHAHIDI WA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA
MANJI AACHIWA HURU KWA KUKOSEKANA USHAHIDI WA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA
Mfanya biashara Yusuf Manji leo Oktoba 6 2017 amefutiwa kesi iliyokuwa ikimkabili ya kutumia dawa za kulevya.
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Cyprian Mkeha baada ya upande wa mashtaka na wa utetezi kufunga ushahidi.
Sababu ambayo imepelekea kufutwa kwa kesi hiyo imetajwa kuwa ni upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha kosa la mtuhumiwa, Yusuf Manji. Katika kesi hiyo, Manji anadaiwa kati ya Februari 6 na 9, 2017 eneo la Sea View, Upanga wilayani Ilala alitumia dawa za kulevya aina ya heroine.
Mahakama imemuachia huru Manji ikiwa ni siku chache tangu shauri lake jingine la Uhujumu uchumi liondolewe Mahakani hapo na Mkurugenzi wa mashitaka (DPP) ambaye alieleza kuwa hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.
Manji amewahi kuwa mwenyekiti wa klabu ya soka ya Yanga ambapo alijiuzulu wadhifa huo mapema mwaka huu.
Pia Manji alikuwa Diwani wa Kata ya Mbagala kabla ya kuvuliwa nafasi hiyo baada ya kupoteza sifa.
Hivyo makala MANJI AACHIWA HURU KWA KUKOSEKANA USHAHIDI WA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA
yaani makala yote MANJI AACHIWA HURU KWA KUKOSEKANA USHAHIDI WA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MANJI AACHIWA HURU KWA KUKOSEKANA USHAHIDI WA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/manji-aachiwa-huru-kwa-kukosekana.html
0 Response to "MANJI AACHIWA HURU KWA KUKOSEKANA USHAHIDI WA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA"
Post a Comment