Mama Maria Nyerere Awaasa Vijana Kuthamini Michezo na Utamaduni

Mama Maria Nyerere Awaasa Vijana Kuthamini Michezo na Utamaduni - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mama Maria Nyerere Awaasa Vijana Kuthamini Michezo na Utamaduni, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mama Maria Nyerere Awaasa Vijana Kuthamini Michezo na Utamaduni
kiungo : Mama Maria Nyerere Awaasa Vijana Kuthamini Michezo na Utamaduni

soma pia


Mama Maria Nyerere Awaasa Vijana Kuthamini Michezo na Utamaduni


PICHA 1
Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO ) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abassi akisikiliza jambo kutoka kwa Mama Maria Nyerere kuelekea kumbukizi ya miaka 18 ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati wa mahojiano maalum na Mjane huyo nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO ) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abassi akifanya mahojiano na Mama Maria Nyerere kuelekea kumbikizi ya Baba wa Taifa , Mjane huyo aliwasisitiza vijana kuzingatia michezo na utamaduni.
Picha na Paschal Dotto- MAELEZO
………..
Na.Paschal Dotto-MAELEZO
12-10-2017.
Mama Maria Nyerere amewaasa vijana kuzingatia utamaduni na michezo ili kuweka sawa akili yao na kuendelea na ujenzi wa taifa kwani michezo hukutanisha watu wengi na kuwawezesha kubadilishana mawazo yenye kujenga katika maisha.
Akizungumza leo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dkt. Hassan Abbasi nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam, Mama Maria Nyerere alisema kuwa michezo ni hatua muhimu ya ukombozi wa fikra kwa vijana kwani wakizingatia michezo wataweza kufanya kazi na kujipatia mahitaji muhumi kama chakula na kuondokana na dhana ya utegemezi.
“Vijana wamajikita katika mambo maovu, sasa kitakachoweza kusaidia ni michezo kwani inawachangamsha, kuwakutanisha na kuweza kubadilishana mawazo mazuri na kwa sasa wanaendelea vyema na masuala haya ya michezo ambayo yanadumisha pia utamaduni,” alisema Mama Maria
Aidha, Mjane wa Hayati Baba wa Taifa alisema kuwa kwa sasa vijana wameanza kujirudi katika kudumisha utamaduni kwani walitaka kupotoka na kuacha utamaduni wao, alieleza kuwa watoto wanazaliwa bila ukomavu wa akili katika utamaduni, lakini pia hawapati elimu ya kutosha kutoka kwa wazazi kuhusu utamaduni matokeo yake ni kuishia kuwa na watu wenye tabia za ajabu.
“Kitakachoweza kuwasaidia vijana wetu ni kuwafundisha utamaduni wetu ili wawe na maadili kwani sasa hivi mtoto anazaliwa hapati elimu ya utamaduni wake, wazazi wametupa utamaduni mbali, ni lazima mtoto atakuwa na tabia za ajabu ajabu,”alisisitiza Mama Maria Nyerere.
Aliongeza  kuwa jukumu la ukombozi wa vijana kutoka katika vitendo vibovu ni la watanzania wote kuweza kuwaelimisha vijana kuhusu michezo ili kuweka akili zao sawa katika kuzalisha na kusaidia kujipatia  kipato chao na taifa kwa ujumla.
Mama Maria Nyerere alisema kuwa kujitegemea kwa vijana hasa katika kufanya kazi kutawawezesha kutimiza ndoto zao na za taifa lenye uchumi wa viwanda kwa ujumla.


Hivyo makala Mama Maria Nyerere Awaasa Vijana Kuthamini Michezo na Utamaduni

yaani makala yote Mama Maria Nyerere Awaasa Vijana Kuthamini Michezo na Utamaduni Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mama Maria Nyerere Awaasa Vijana Kuthamini Michezo na Utamaduni mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/mama-maria-nyerere-awaasa-vijana.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Mama Maria Nyerere Awaasa Vijana Kuthamini Michezo na Utamaduni"

Post a Comment