title : MAKANDARASI KUKUTANA JIJINI DAR, KUJADILI MAENDELEO YA UKUAJI WA VIWANDA
kiungo : MAKANDARASI KUKUTANA JIJINI DAR, KUJADILI MAENDELEO YA UKUAJI WA VIWANDA
MAKANDARASI KUKUTANA JIJINI DAR, KUJADILI MAENDELEO YA UKUAJI WA VIWANDA
Na.Paschal Dotto-MAELEZO.
Chama cha Makandarasi (CATA) kinachounganisha wakandarasi wote nchini kinatarajia kukutana Novemba 17, 2017 kujadili kuhusu ukuaji wa viwanda nchini mkutano utakaofanyika katika ukumbi wa Diamondi Jubilee Jijini Dar es Salaam.
Akizungumuza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Mhandisi Lawrence Mwakyambiki alisema kuwa Serikali ya Aawamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais John Pombe Magufuli iko kwenye njia ya ujenzi wa viwanda kwa hiyo sekta ya ujenzi inahitajika kwa kiasi kikubwa kwenye sera hii ya viwanda.
“Lengo la mkutano huu kwa wakandarasi hawa ni kutaka kuleta mchango wao katika ujenzi wa uchumi wa Tanzania na wameona kwamba kama wazawa wanaowajibu wa kutoa mchango katika katika ujenzi wa viwanda nchini”, alisema Mhandisi Mwakyambiki.
Aidha Mhandisi Mwakyambiki aliseka kuwa katika maendeleo ya taifa tasnia ya ujenzi ni muhimu kwani inabeba vitu vingi na kuwawezesha wananchi kupata huduma stahiki kama elimu na afya na kuwataka makandarasi kufanya kazi zo kwa ufanisi mkubwa.
Mwenyekiti wa Chama cha Makandarasi Mhandisi Lawrence Mwakyambiki (katikati) akieleza jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) katika utambulisho wa mkutano wa chama hicho utakaofanyika Novemba 17, 2017 Diamondi Jubilee Jijini Dar es Salaam,kulia ni Meneja Mauzo wa benki ya cba Bi.Kunenguda Dedede na kushoto ni Mkuu wa Masoko kutoka NMB Bi.Linda Teggisa.
Meneja Mauzo wa benki ya cba Bi.Kunenguda Dedede akieleza jambo kwa waandishi wa habari( hawapo pichani) kuhusu mkutano wa makandarasi hapo novemba 17, 2017 katika ukumbi wa diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam, wa kwanza kushoto ni Mkuu wa masoko kutoka NMB Bi.Linda Teggisa na Mwenyekiti wa Chama cha Makandarasi Mhandisi Lawrence Mwakyambiki.(Picha na Paschal Dotto-MAELEZO).
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala MAKANDARASI KUKUTANA JIJINI DAR, KUJADILI MAENDELEO YA UKUAJI WA VIWANDA
yaani makala yote MAKANDARASI KUKUTANA JIJINI DAR, KUJADILI MAENDELEO YA UKUAJI WA VIWANDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAKANDARASI KUKUTANA JIJINI DAR, KUJADILI MAENDELEO YA UKUAJI WA VIWANDA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/makandarasi-kukutana-jijini-dar.html
0 Response to "MAKANDARASI KUKUTANA JIJINI DAR, KUJADILI MAENDELEO YA UKUAJI WA VIWANDA"
Post a Comment