title : Homa Ini Bado Waendelea Kuwa Tishio
kiungo : Homa Ini Bado Waendelea Kuwa Tishio
Homa Ini Bado Waendelea Kuwa Tishio
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imetoa ripoti ya robo mwaka tangu ianze kufanya uchunguzi wa Virusi vya Homa ya Ini ( Hepatitis B) na kutoa tiba ya ugonjwa huo kwa kutumia dawa ya Tenofovir .
Akitoa taathimini hiyo leo jijini Dar es salaam, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ini na Matumbo John Rwegasha amesema muamko ni mkubwa ambapo katika kipindi cha robo mwaka , Hospitali ya Taifa Muhimbili imesajili wagonjwa 950 .
Akifanunua amesema hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu idadi ya wagonjwa itaongezeka na kufika 1800 .Hata hivyo kati ya hao , wagonjwa 540 ndio wamerudi tena Hospitalini kwa ajili ya kuendelea na mchakato wa uchunguzi huku wagonjwa wengine wakishindwa kufika kutokana na sababu za mbalimbali hususani za kiuchumi , nakuongeza kwamba waliopo kwenye tiba ni wagonjwa 40.
‘’Idadi ya wagonjwa imeongezeka mara dufu hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu watafika wagonjwa 1800 lakini pamoja na changamoto hiyo hatuwezi kusimamisha huduma tutaendelea kutoa huduma kwani kwa upande wa dawa tumejidhatiti kwa miaka mitano , wagonjwa hawa wanatakiwa wafanyiwe uchunguzi ili aanze kutumia dawa lakini si wote wanaohitaji dawa’’ amesema DK. Rwegasha.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba katika hospitali hiyo, Dk. Hedwiga Swai akisisitiza watu kujitokeza kupima afya ili kuthibiti homa ya ini pamoja na magonjwa mengine.
Daktari Bingwa wa Magomjwa ya Mfumo wa Chakula na Ini, John Rwegasha wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akizungumza katika kongamano jinsi ya kudhibiti na kutibu magonjwa ya mfumo wa chakula na ini.
Baadhi ya watumishi wa hospitali hiyo wakiwamo madaktari na wauguzi wakifuatilia kongamano hilo.
Hivyo makala Homa Ini Bado Waendelea Kuwa Tishio
yaani makala yote Homa Ini Bado Waendelea Kuwa Tishio Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Homa Ini Bado Waendelea Kuwa Tishio mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/homa-ini-bado-waendelea-kuwa-tishio.html
0 Response to "Homa Ini Bado Waendelea Kuwa Tishio"
Post a Comment