Chama cha Wasafirishaji Tanzania chazungumzia kero za wanachama wake

Chama cha Wasafirishaji Tanzania chazungumzia kero za wanachama wake - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Chama cha Wasafirishaji Tanzania chazungumzia kero za wanachama wake, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Chama cha Wasafirishaji Tanzania chazungumzia kero za wanachama wake
kiungo : Chama cha Wasafirishaji Tanzania chazungumzia kero za wanachama wake

soma pia


Chama cha Wasafirishaji Tanzania chazungumzia kero za wanachama wake

Makamu wa Rais wa Chama cha Wasafirishaji Tanzania (TAT), Omar Kiponza akizungumza na vyombo vya habari kuelezea kero mbalimbali zinazowakabili wanachama wake leo katika ofisi za chama hicho jijini Dar es Salaam.

CHAMA CHA WASAFIRISHAJI TANZANIA (TAT)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ukumbi wa Mikutano wa TAT
Ofisi ya TAT Bamaga.

Kwa niaba ya bodi ya chama cha wasafirishaji na kama tulivyokubaliana wiki moja iliyopita, tunapenda kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusiana na mambo kadhaa ambayo yamekuwa yakijitokeza Katika shughuli za kila siku za wanachama wetu na kumekuwa na malalamiko mengi ambayo yamekuwa yakitolewa na kuhusiana na kero hizo.

Hivyo kama chama cha wasafirishaji tumeonelea ni vyema tukayaweka mambo haya bayana ili vyombo husika viweze kuchukua hatua ili kuwawezesha wanachama wetu kufanya biashara zao bila usumbufu na kupunguza gharama ambazo hazina tija Katika uendeshaji wa biashara hii usafirishaji wa mizigo ndani na nje ya nchi.
Malalamiko hayo ni kama ifuatavyo :-

Tungependa kutoa malalamiko haya kwa TANROADS kuhusiana na maegesho yaliyopo Katika baadhi ya barabara ambazo magari ya wanachama wetu yamekuwa yakipitia kila siku Katika barabara hizo na ukiangalia hakuna sehemu maalum ya maegesho hivyo utaratibu unaotumiwa kuvuta magari bila ridhaa sababu wamekuwa wakivuta magari bila kutaka maelezo hata kama gari linaweza kutembea lenyewe na kosa kubwa wanalosema ni kwamba umepaki kwenye road reserve hata kama dereva amesimama kwa ajili ya dharura ya posho au document wanakuambia gari iondolewa iende misugusugu na fine wanazotoza huwa ni kubwa mno.ikiwa mwanachama wetu atafanya gereji Barabarani au kufunga njia kwa uzembe basi hapo hatuna pingamizi lolote sheria ifuate mkondo wake na hatuwezi kutetea uharibifu wa miundombinu ya nchi yetu.

Vile vile kuna suala la mzani ambao upo nje ya Bandari kutokana na usumbufu ambao wanachama wetu wanaoupata endapo mzigo umezidi na unatakiwa kupangwa upya hivyo  tunaomba mamlaka husika ambao ni TANROADS watusaidie kwenye hili suala ikiwezekana huu mzani uwekwe ndani ya Bandari.

Wakati wa kupakia na kushusha mizigo Bandarini na kwenye Bandari kavu pia kumekuwa na usumbufu huu na kumekuwa na sintofahamu kubwa juu ya nani mwenye barabara hizi kwa sababu kuna wakati wanakuja watu wa manispaa wanasema wrong parking na wakati mwingine TANROADS pia wanasema umepaki gari vibaya sasa hatuelewi kukinzana kwa mamlaka mbili Katika suala moja la maegesho inakuaje utaratibu huu.

Kuna suala la mizani kutofanyiwa calibration hili suala limekuwa likizunguziwa kwa muda mrefu sana na mizani mingi haina uwiano Katika usomaji tunawaomba muliangalie suala hili kwa umakini ili sote tufanye kazi kama marafiki.

Upande wa mamlaka ya mapato Tanzania yaani TRA pia kumekuwa na kero ambayo wanachama wetu wanapenda kutoa malalamiko hii ni juu ya suala la utozaji wa faini ya shilingi elfu 40,000 endapo gari litakuwa halijavuka mpaka ndani ya siku7 pale tunduma ikifika siku ya 8 TRA Wanaanza kutoza chaji hiyo kwa kosa ambalo si la msafirishaji.

Vile kuna jambo ambalo limezuka toka SUMATRA ambapo kuna baadhi ya wanachama wetu wananunua trailers au gari ya mtumba tangia mwaka jana 2016 ambayo haijawahi kufanya kazi hapa nchini lakini wakati wa kwenda kuomba leseni ya usafirishaji kumekuwa na hii kero ya kutozwa faini kwa kitu ambacho hakijawahi kutembea kwa kisingizio kuwa faini hiyo ni kwa ajili ya part registration sasa faini ya nini kwa kitu ambacho hakijatumika?

Vivyo hivyo kuna jambo lingine linalohusisha watu wa maliasili pindi magari yanapopakiwa mkaa na madereva siyo kwa ruhusa ya tajiri lakini wanapokamatwa adhabu yote ya faini analipishwa tajiri wakati huo huo dereva hapewi adhabu yoyote je hii ni sawa kweli,kwa sababu kuna wasafirishaji ambao washapigwa faini kama milioni 24 kwa sababu ya mkaa je mamlaka husika wanafahamu hili au ni sheria watu wanajichukulia mikononi. 

Mwisho kabisa tungependa kutoa shukrani za dhati kwa Mstahiki Meya wa jiji,Mkurugenzi wa jiji, wakurugenzi wa Manispaa wa wilaya zote,Mratibu wa Maegesho wa jiji kwa kuondoa kero ya madalali waliokuwa wakikamata magari kwa uonevu tunatumai huu ni mwanzo mzuri kwa hatua kama hizi kuchukuliwa na tunahakika serikali yetu ipo makini Katika kuhakikisha wananchi wake wanasikilizwa pale panapokuwa na walakini Katika utendaji na uendeshaji wa shughuli za kila siku.

KATIBU


Hivyo makala Chama cha Wasafirishaji Tanzania chazungumzia kero za wanachama wake

yaani makala yote Chama cha Wasafirishaji Tanzania chazungumzia kero za wanachama wake Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Chama cha Wasafirishaji Tanzania chazungumzia kero za wanachama wake mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/chama-cha-wasafirishaji-tanzania.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Chama cha Wasafirishaji Tanzania chazungumzia kero za wanachama wake"

Post a Comment