WAZIRI TZEBA AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKUU WA (FAO) JOSÉ GRAZIANO DA SILVA JIJINI DAR ES SALAAM

WAZIRI TZEBA AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKUU WA (FAO) JOSÉ GRAZIANO DA SILVA JIJINI DAR ES SALAAM - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI TZEBA AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKUU WA (FAO) JOSÉ GRAZIANO DA SILVA JIJINI DAR ES SALAAM, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI TZEBA AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKUU WA (FAO) JOSÉ GRAZIANO DA SILVA JIJINI DAR ES SALAAM
kiungo : WAZIRI TZEBA AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKUU WA (FAO) JOSÉ GRAZIANO DA SILVA JIJINI DAR ES SALAAM

soma pia


WAZIRI TZEBA AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKUU WA (FAO) JOSÉ GRAZIANO DA SILVA JIJINI DAR ES SALAAM


Na Mathias Canal, Dar es salaam

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silva, leo Jumanne Septemba 5, 2017 amefanya mazungumzo na waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya kikazi nchini Tanzania. 

Katika ziara hiyo Bw. Graziano da Silva atafanya mazungumzo na viongozi waandamizi wa Serikali, wadau na anatarajiwa kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein sambamba na Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed.

Ziara hii ya Mkurugenzi Mkuu inajili wakati FAO ikiadhimisha miaka 40 toka kuanza shughuli zake hapa Tanzania Hafla ambayo itahudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Samia Suluhu Hassan. 

Katika mazungumzo na Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mkurugenzi Mkuu wa FAO anabadilishana mawazo na Serikali ya Muungano wa Tanzania kwenye masuala makuu yanayohusiana na uhakika wa chakula na maendeleo ya kilimo, ikijumuisha juhudi za FAO kitaifa na kikanda.

Pia yamejadiliwa mambo mengine yanayohusiana na ushirikiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na FAO, pia masuala ya umuhimu kati ya pande hizo mbili.Mbali ya Maafisa wa Serikali, Mkurugenzi Mkuu atakutana na wadau wengine wa FAO hapa nchini wakiwa ni pamoja na asasi za kiraia, taasisi za elimu, na taasisi za utafiti. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silva (Kulia), akimpongeza Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba mara baada ya kuelezea taarifa mbalimbali zihusuzo wizara hiyo. leo Jumanne Septemba 5, 2017.
Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silva, kuzungumzia ujio wake nchini na ushirikiano baina ya FAO na serikali ya Tanzania. leo Jumanne Septemba 5, 2017.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silva, akizungumzia na wataalamu mbalimbali katika Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi juu ya ujio wake nchini na ushirikiano baina ya FAO na serikali ya Tanzania. Kulia kwake ni Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba. leo Jumanne Septemba 5, 2017.
Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba akipokea simu 50 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silvakwa ajili ya wataalamu wa kilimo kuzitumia kukusanya taarifa mbalimbali na kuziwasilisha kwa jamii. leo Jumanne Septemba 5, 2017.
Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba akionyesha moja ya siku kati ya 15 alizokabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silva kwa ajili ya wataalamu wa kilimo kuzitumia kukusanya taarifa mbalimbali na kuziwasilisha kwa jamii. leo Jumanne Septemba 5, 2017.



Hivyo makala WAZIRI TZEBA AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKUU WA (FAO) JOSÉ GRAZIANO DA SILVA JIJINI DAR ES SALAAM

yaani makala yote WAZIRI TZEBA AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKUU WA (FAO) JOSÉ GRAZIANO DA SILVA JIJINI DAR ES SALAAM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI TZEBA AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKUU WA (FAO) JOSÉ GRAZIANO DA SILVA JIJINI DAR ES SALAAM mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/waziri-tzeba-afanya-mazungumzo-na.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI TZEBA AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKUU WA (FAO) JOSÉ GRAZIANO DA SILVA JIJINI DAR ES SALAAM"

Post a Comment