title : WAZIRI MKUU ATOA MSAADA WA SH. MILIONI 10
kiungo : WAZIRI MKUU ATOA MSAADA WA SH. MILIONI 10
WAZIRI MKUU ATOA MSAADA WA SH. MILIONI 10
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa msaada wa sh. milioni 10 ili kumuwezesha Bw. Ernest Masenga kutatua changamoto zinazomkabili. Masenga alikuwa msanii wa muziki wa dansi ambaye sasa anasumbuliwa na maradhi ya miguu. Pia makazi anayoishi si salama yanahitaji kukarabatiwa.
Waziri Mkuu ametoa msaada huo leo (Jumatatu, Septemba 11, 2017) katika makazi ya Waziri Mkuu Oysterbay jijini Dar Es Salaam. Ametoa msaada huo baada ya kuguswa na hali ya maisha ya msanii huyo aliyemuona kupitia kipindi maalumu kilichoonyeshwa na TBC Septemba, 5, 2017. Kipindi hicho kiliongozwa na Godfrey Nago.
“Nawaomba Watanzania wenzangu tumsaidie mwezetu ili aweze kuishi vizuri kwa sababu sanaa yake imesaidia katika kuelimisha na kuburudisha umma .”
Kwa upande wake Nago ambaye amepokea msaada huo kwa niaba ya Masenga amesema atahakikisha anasimamia vizuri fedha hizo ili zitumike kama ilivyokusudiwa.
Pia Nago amesema anamshukuru Waziri Mkuu kwa kuwaunga mkono na kutoa msaada huo kwa sababu ameonesha kwamba Serikali inawajali wananchi wake na TBC itaendelea kuwaomba wadau mbalimbali wajitokeze na kumsaidia msanii huyo.
Naye Mjomba wa msanii huyo, Kanuti Mloka ambaye ameiwakilisha familia amemshukuru Waziri Mkuu kwa msaada huo kwa kuwa familia imeshindwa kumsaidia Bw. Masenga kutokana hali duni ya maisha waliyonayo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikabidhi msaada wa sh. milioni 10 kwa Meneja wa TBC 2, Godfrey Nago ili kumsaidia Msanii wa muziki wa dansi, Ernest Masenga. Nago amepokea kwa niaba ya msanii huyo. Kushoto ni mjomba wa msanii huyo, Kanuti Mloka. Makabidhiano hayo yamefanyika leo Septemba 11/2017 katika ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dar es salaam.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Hivyo makala WAZIRI MKUU ATOA MSAADA WA SH. MILIONI 10
yaani makala yote WAZIRI MKUU ATOA MSAADA WA SH. MILIONI 10 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU ATOA MSAADA WA SH. MILIONI 10 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/waziri-mkuu-atoa-msaada-wa-sh-milioni-10.html
0 Response to "WAZIRI MKUU ATOA MSAADA WA SH. MILIONI 10"
Post a Comment