title : Warembo vyuo vikuu kupambana Septemba 29
kiungo : Warembo vyuo vikuu kupambana Septemba 29
Warembo vyuo vikuu kupambana Septemba 29
Warembo wa vyuo vikuu vya Tanzania “Miss Higher Learning Institution 2017” watapanda jukwaani Septemba 29, kwenye ukumbi wa King Solomoni, Namanga jijini. Mashindano hayo yameandaliwa na kampuni ya Glamour Bridal Tanzania baada ya kupewa idhini ya waandaaji wa Miss Tanzania, Lino International Agency kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa Tanzania (Basata).
Mkurugenzi wa Glamour Bridal Tanzania Muba Saedo alisema kuwa wanatarajia kufanya mashindano yenye upinzani wa hali ya juu kutokana na idadi ya vyuo mbalimbali vilivyothibitisha.
Mbali ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii (ISW), mashindano hayo yatashirikisha vyuo vya Taasisi ya Uhasaibu Dar es Salaam (TIA), IFM, CBE, UDOM, Tumaini – Makumira na Taasisi ya Uhasibu wa Arusha (IAA) na Chuo Kikuu Cha Ardhi.
Saedo alivitaja vyuo vingine kuwa ni Mzumbe, Chuo Kikuu cha Iringa, Tanzania Aviation University College na Magogoni. Alisema kuwa bado wanapokea maombi kutoka vyuo mbalimbali na mwisho wa kuthibitisha ni Septemba 11.
“Kwa sasa tunapokea warembo ili kuweza kushiriki katika mashindano haya, kuna vyuo vilifanya mashindano na vingine vilifanya uteuzi wa ndani na kutuletea majina kutokana na kuepuka gharama za kufanya mashindano,”
“Mpaka sasa kuna warembo ambao wamejitokeza kuwania nafasi tatu za kushiriki mashindano ya Miss Tanzania mwaka huu, kwa vile tunahitaji mashindano bora yenye ushindani wa hali ya juu, bado tunawakaribisha wasichana wanaosoma vyuo mbalimbali kuwasiliana na waandaaji ili kujaribu bahati yao,” alisema Saedo.
Kwa mujibu wa Saedo warembo wanaotaka kushiriki katika mashindano hayo wanatakiwa kuomba kupitia instagram page @higher_learning_miss_tz_2017 au kupitia mubasaedo4me@gmail.com, msaedo@glamourbridal@gmail.co.tz na jmsendo@glamourbridal.co.tz.
Miss Higher Learning Institutions 2016 , Laura Kwai akipunga mkono baada ya kutangazwa kutwaa taji hilo kwenye Ukumbi wa King Solomoni jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mshindi wa pili Evelyn Andrew pamoja na mshindi wa tatu Clara Nyaki.
Hivyo makala Warembo vyuo vikuu kupambana Septemba 29
yaani makala yote Warembo vyuo vikuu kupambana Septemba 29 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Warembo vyuo vikuu kupambana Septemba 29 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/warembo-vyuo-vikuu-kupambana-septemba-29.html
0 Response to "Warembo vyuo vikuu kupambana Septemba 29"
Post a Comment