title : WADAU WA ELIMU WAKUTANA KUADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA KISOMO,JIJINI DAR
kiungo : WADAU WA ELIMU WAKUTANA KUADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA KISOMO,JIJINI DAR
WADAU WA ELIMU WAKUTANA KUADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA KISOMO,JIJINI DAR
Wadau mbalimbali wa elimu wamekutana kuadhimisha siku ya kimataifa ya kisomo ambayo hufanyika Septemba 8 kila mwaka. Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na taasisi ya iSwapMyBooks kwa kushirikiana na SOMA pia Elimika Wikiendi ulihusisha mjadala wa namna ambavyo Tanzania inaweza kutumia faida ya uwepo wa nyenzo za kidigitali katika kusaidia watoto na watu wazima kujifunza.
Akifungua maadhimisho hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya SOMA Bi. Demere Kitunga alieleza namna ambavyo kwa miaka ya karibuni Tanzania imekuwa ikipiga hatua katika matumizi ya nyenzo za kiditali kutokana na usambaaji wa matumizi ya vifaa vilivyounganishwa na mtandao wa intaneti hivyo kupelekea uhitaji katika kutumia nyenzo hizi katika kuboresha namna ambavyo watoto wanaweza kujifunza masomo.
Wanajopo walioshiriki mjadala huo Irene Kiwia wa TWA network, Given Edward toka mtandao wa MyElimu, Kiya JK wa taasisi ya SEMA na Viola Julius mratibu wa tovuti ya iSwapMyBooks walielezea namna ambavyo taasisi zao zimekuwa zikitumia njia za kidigitali kuwahamasisha watoto na vijana kujifunza kwa kubadilishana ujuzi kupitia mtandaoni.
Washiriki wengine kwa namna tofauti walionyesha wasiwasi kwa namna ambavyo utaratibu wa watu kujisomea unaendelea kutoweka na hasa kwa wazazi ambao wamekuwa hawana utaratibu wa kuwanunulia watoto vitabu badala yake kuwapa simu za mkononi ambazo wamekuwa wakizitumia kwa mambo yasiyofaa.
Wanajopo walioshiriki mjadala huo kutoka kushoto ni Viola Julius mratibu wa tovuti ya iSwapMyBooks, Given Edward toka mtandao wa MyElimu,Kiya JK wa taasisi ya SEMA na Irene Kiwia wa TWA network
Mmoja wa wachangiaji Bw. Yeriko Nyerere akichangia jambo wakati wa siku hiyo
Bw. Paschal Masalu kutoka Elimika Wikiendi akiendelea ku Tweet wakati wa Siku hiyo ya kisomo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WADAU WA ELIMU WAKUTANA KUADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA KISOMO,JIJINI DAR
yaani makala yote WADAU WA ELIMU WAKUTANA KUADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA KISOMO,JIJINI DAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WADAU WA ELIMU WAKUTANA KUADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA KISOMO,JIJINI DAR mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/wadau-wa-elimu-wakutana-kuadhimisha.html
0 Response to "WADAU WA ELIMU WAKUTANA KUADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA KISOMO,JIJINI DAR"
Post a Comment