Uongozi mpya wa TFF watembelea SBL

Uongozi mpya wa TFF watembelea SBL - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Uongozi mpya wa TFF watembelea SBL, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Uongozi mpya wa TFF watembelea SBL
kiungo : Uongozi mpya wa TFF watembelea SBL

soma pia


Uongozi mpya wa TFF watembelea SBL

Mwambawahabari


Rais wa TFF ,Wallace Karia akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani
alipofanya ziara katika Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) ambayo ni wadhamini wakuu wa Timu ya Taifa, Taifa Stars.pembeni yake kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Helene Weesie na kulia ni Mkurungezi wa masoko wa SBL Ceaser Mloka na mwishoni ni Kocha mkuu wa Taifa stars Salum Manyanga,Mapema jana katika ofisi za makao makuu ya SBL Temeke Jijini Dar es salaam.

ya wa TFF ikiwa ni wiki moja kabla ya mechi ya kirafiki ya kimataifa itakayozikutanisha Taifa Stars na Malawi, mchezo utakaofanyika  kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. Tangu imepata udhamini wa SBL mwezi Mei mwaka huu, Taifa Stars imecheza mechi nne za kimataifa na kufanikiwa kuweka rekodi nzuri kwenye mechi zote ilizocheza.
 
Akiongea wakati wa ziara hiyo, Rais wa mpya wa TFF aliishukuru SBL kwa udhamini wake kwa timu ya taifa na aliihakikishia SBL kuwa uongozi wake umeunda  menejimenti ya Taifa Stars ili kuhakikisha kuwa timu ya taifa inapata ushindi kwenye kila mechi.
 
“Tunaishukuru SBL kwa kutoa msaada uliokuwa unahitajika sana na ambao umeiwezesha timu yetu ya taifa kujiandaa vyema na mechi na kufanya vizuri kwa ngazi ya kitaifa na kimataifa,” alisema Karia
 
Karia alisisitiza kuwa fedha zilizotolewa kwa ajili ya udhamini wa timu ya taifa, zitatumika vizuri na kuongeza kuwa uongozi wa TFF unalenga kuongeza imani kwa wadhamini wa Taifa Stars na wadau wa soka kwa ujumla wake.
 
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Helene Weesie alimpongeza Rais mpya wa TFF pamoja na timu yake kwa kuchaguliwa na kueleza kuwa SBL itaendelea kutoa misaada inayolenga kuendeleza michezo hapa nchini.
“SBL inatambua mchango muhimu ambao michezo inatoa kwenye maendeleo ya kiuchumi na kijamii na ndiyo maana tunaamini kuwa tunapoidhamini Taifa Stars, tunachangia katika kuwaburudisha na kuwaunganisha Watanzania wakiwa na bia yao bora ya Serengeti ikwa na ujumbe wake wa sifa yetu, bia yetu, nchi yetu,” alisema
 
Mwezi Mei mwaka huu, TFF iliingia mkataba wa ufadhili kwa Taifa Stars utakaodumu kwa kipindi cha miaka 3 utagharimu shilingi blioni 2.1na kuifanya SBL kuwa mdhamini mkuu wa timu ya taifa.
 
Ikizalishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1996, bia ya Serengeti imetengenezwa na kimea kwa asilimia 100 huku ikiweza kushinda tuzo zaidi ya 10 kwa ngazi ya kitaifa na kimataifa kutokana na ubora wake wa kimataifa.


Hivyo makala Uongozi mpya wa TFF watembelea SBL

yaani makala yote Uongozi mpya wa TFF watembelea SBL Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Uongozi mpya wa TFF watembelea SBL mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/uongozi-mpya-wa-tff-watembelea-sbl.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Uongozi mpya wa TFF watembelea SBL"

Post a Comment