THE DESK & CHAIR YAWAPIGA JEKI WATOTO 50 GHARAMA ZA MATIBABU

THE DESK & CHAIR YAWAPIGA JEKI WATOTO 50 GHARAMA ZA MATIBABU - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa THE DESK & CHAIR YAWAPIGA JEKI WATOTO 50 GHARAMA ZA MATIBABU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : THE DESK & CHAIR YAWAPIGA JEKI WATOTO 50 GHARAMA ZA MATIBABU
kiungo : THE DESK & CHAIR YAWAPIGA JEKI WATOTO 50 GHARAMA ZA MATIBABU

soma pia


THE DESK & CHAIR YAWAPIGA JEKI WATOTO 50 GHARAMA ZA MATIBABU

NA BALTAZAR MASHAKA,MWANZA
TAASISI ya The Desk & Chair Foundation (TD&CF) imekabidhi hundi mbili zenye thamani ya zaidi sh. 2.5 kwa vituo vya Karibu Foundation na Nitetee Foundation ili kuwawezesha  watoto 50 wanaolelewa kwenye vituo hivyo kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF).
Akizungumza jana baada ya kukabidhi hundi hizo Mwenyekiti wa TD & CF Sibtain Meghjee alisema fedha hizo zitatumika kugharamia matibabu ya watoto hao kwa kipindi cha mwaka mmoja.
“ Watoto wanaolelewa kwenye vituo vya Nitetee Foundation na Karibu Foundation,  wengi wao wanatoka kwenye familia duni na wanaishi katika mazingira magumu.Tumeona tuwasaidie kwa kuwakinga na magonjwa kwa kuwalipia mchango wa uanachama wa Bima ya Afya wa sh. 54,000 utakaomuwezesha mtoto kutibiwa kwa mwaka mzima ambapo kila kituo kimepewa sh. 1, 260,000 kwa ajili ya watoto 25 ambao wamesajiliwa tayari, ”alisema. 
 Meneja wa kituo cha Nitetee Foundation, Johaness Emmanuel akipokea hundi ya sh. 1,260,000 za malipo ya mchango wa uanachama wa bima ya afya kwa watoto 25 wa kituo hicho kutoka kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyamagana, kulia mwenye kinasa sauti ni Mwenyekiti wa Taasisi ya The Desk & Chair Foundation Tawi la Tanzania Sibtain Meghjee ambayo imetoa fedha hizo kwa kituo hicho na Karibu Foundation.Kulia mwenye shati ya draft ni Meneja Matekelezo wa NHIF Mkoa wa Mwanza Calistus Mpangala. Picha ya Baltazar Mashaka.
 Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) Mkoa wa Mwanza, Castus Mpangala akitoa ufafanuzi wa huduma zinazotolewa na mfuko huo kwa wananchi waliohudhuria semina ya bima ya afya iliyoandaliwa na Taasisi ya The Desk & Chair Foundation Tawi la Tanzania ili kuwahamasisha  kujiunga na mfuko huo kwa ajili ya kupata matibabu kwa gharama nafuu. Semina hiyo ilifanyika jijini Mwanza.
 Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella mwenye kofia akiwa ameshika moja ya mashuka yaliyotolewa msaada na Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) Mkoa wa Mwanza kwa Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe. Wa tatu kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dk.Leonard Subi, Meneja wa mfuko huo mkoani Mwanza Dk. Mohamed Kilolile wanne kulia na  kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Uekerewe Estomiah Chang'a.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella (mwenye kofia) hivi karibuni akinunua samaki aina ya Furu kutoka kwa akinamama wachuuzi wa samaki katika Soko la Kakukulu lililopo wilayani Ukerewe. Mkuu huyo wa Mkoa alikuwa wilayani humo kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali. Picha na Baltazar Mashaka.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA



Hivyo makala THE DESK & CHAIR YAWAPIGA JEKI WATOTO 50 GHARAMA ZA MATIBABU

yaani makala yote THE DESK & CHAIR YAWAPIGA JEKI WATOTO 50 GHARAMA ZA MATIBABU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala THE DESK & CHAIR YAWAPIGA JEKI WATOTO 50 GHARAMA ZA MATIBABU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/the-desk-chair-yawapiga-jeki-watoto-50.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "THE DESK & CHAIR YAWAPIGA JEKI WATOTO 50 GHARAMA ZA MATIBABU"

Post a Comment