title : TAASISI YA TACC YATOA MAFUNZO KWA VIJANA WAJASIRIAMALI WILAYANI KIABAHA YA KUWAJENGEA UWEZO KATIKA KUPAMBANA NA SOKO LA AJIRA
kiungo : TAASISI YA TACC YATOA MAFUNZO KWA VIJANA WAJASIRIAMALI WILAYANI KIABAHA YA KUWAJENGEA UWEZO KATIKA KUPAMBANA NA SOKO LA AJIRA
TAASISI YA TACC YATOA MAFUNZO KWA VIJANA WAJASIRIAMALI WILAYANI KIABAHA YA KUWAJENGEA UWEZO KATIKA KUPAMBANA NA SOKO LA AJIRA
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA .
VIJANA wajasiriamali zaidi ya 50 kutoka Wilayani Kibaha Mkoa Pwani wamepatiwa mafunzo kwa lengo la kuweza kujifunza stadi mbali mbali za maisha pamoja na namna ya kuweza kujiajiri wao wenyewe kupitia biashara ndogo ndogo wanazozifanya ili kuweza kupambana na wimbi la umasikini na kujikwamua kiuchumi kwa lengo la kuweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo.
Mafunzo hayo ya vijana ambayo yanafanyika mjini Kibaha kwa muda wa siku 14 yameandaliwa na Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya ushindani na biashara Tanzania (TECC) kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wa maendeleo kwa lengo la kuweza kuwawezesha vijana hao ili waweze kupambana na changamoto inayowakabili kwa sasa ya upatikanaji wa soko la ajira.
Akizungumza katika uzinduzi wa programu hiyo ya kuwasaidia vijana wajasiliamari Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi hiyo ya TECC Sosthenes Sambua amesema kwamba lengo lao kubwa ni kuhakikisha kwamba inawakomboa vijana hao kwa kuwajengea uwezo wa kuweza kujikwamua kimaisha.
Naye Meneja wa Shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo (SIDO) Mkoa wa Pwani Agnes Yesaya amesema lengo lao kubwa ni kuhakikisha inatoa mafunzo zaidi kwa vijana waliopo katika vikundi mbali mbali pamoja na kuwapatia mikopo pamoja na kuwajengea uwezo kwa ajili ya kuanzisha viwanda vidogo ambayo itaweza kuwapa fursa ya kujiendeleza zaidi katika kukuza mitaji yao.
“Sisi kama sido Mkoa wa Pwani lengo letu kubwa ni kuhakikisha kwamba tunawasaidia vijana katika kuwapatia mafunzo mbali mbali ya ujasiriamali pamoja na stadi za maisha kwa lengo la kuweza kupambana na ajira, hivyo tunatarajia baada ya mafunzo haya yataweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa vijana wetu ikiwemo kupambana na wimbi la umasikini.,”alisema Yesaya.
Meneja wa shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo (SIDO) Mkoa wa Pwani Agnes Yesaya akizungumza jambo mara baada ya uzinduzi wa progamu ya kuwasaidia mafunzo mbali mbali vijana wajasiriamali zaidi ya 50 kutoka Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani (PICHA NA VICTOR MASANGU)
Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya TECC, Sosthenes Sambua ambao ndio waandaaji wa mafunzo hayo ya vijana akizungumzia kuhusina na mikakati ya kuwawezesha vijana hao ili waweze kutimiza ndoto zao mara baada ya kupatiwa ujuzi katika mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki katika mafunzo hayo wakiwa wametulia kwa ajili ya kusikiliza mafunzo ya ujasiliamali.
Mmoja wa vijana wajasiriamali akizungumza na baadhi ya wenzake katika mafunzo hayo kuhusina na jinsi alivyoweza kupata fursa ya kuweza kujiajiri yeye mwenyewe na kupitia mafunzo aliyoyapata hayo awali.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU).
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala TAASISI YA TACC YATOA MAFUNZO KWA VIJANA WAJASIRIAMALI WILAYANI KIABAHA YA KUWAJENGEA UWEZO KATIKA KUPAMBANA NA SOKO LA AJIRA
yaani makala yote TAASISI YA TACC YATOA MAFUNZO KWA VIJANA WAJASIRIAMALI WILAYANI KIABAHA YA KUWAJENGEA UWEZO KATIKA KUPAMBANA NA SOKO LA AJIRA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TAASISI YA TACC YATOA MAFUNZO KWA VIJANA WAJASIRIAMALI WILAYANI KIABAHA YA KUWAJENGEA UWEZO KATIKA KUPAMBANA NA SOKO LA AJIRA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/taasisi-ya-tacc-yatoa-mafunzo-kwa.html
0 Response to "TAASISI YA TACC YATOA MAFUNZO KWA VIJANA WAJASIRIAMALI WILAYANI KIABAHA YA KUWAJENGEA UWEZO KATIKA KUPAMBANA NA SOKO LA AJIRA"
Post a Comment