title : TAMISEMI YATENGA BILIONI MOJA
kiungo : TAMISEMI YATENGA BILIONI MOJA
TAMISEMI YATENGA BILIONI MOJA
Na Silvia Hyera
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo amesema kuwa TAMISEMI imetenga bajeti ya Shilingi Bilioni 1 katika mpango wa lishe wa mwaka 2017/18 wenye lengo la kupeleka agenda ya lishe kitaifa na kutokomeza udumavu na utapia mlo nchini.
Mhe. Jafo alisema hayo jana kwenye mkutano wa nne wa wadau wa sekta ya lishe katika kufanya mapitio ya mpango jumuishi wa lishe 2016/17- 2020/2021 wenye kauli mbiu ya lishe bora ni msingi wa maendeleo ya viwanda nchini Tanzania , uliofanyika katika ukumbi wa mikutano Hazina Mjini Dodoma.Alisema kuwa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI)
Imepewa jukumu la kuratibu mpango wa lishe katika ngazi za Mkoa na Wilaya hivyo mpango huo utatekelezeka kwa kina na uweledi mkubwa katika kuboresha lishe nchini kupitia dhana ya ugatuaji wa madaraka.
“ Tumejielekeza vya kutosha katika kuboresha afya ya kila mtoto, bajeti ya awali ilikuwa shilingi 500 kwa kila mtoto chini ya miaka 5 lakini katika bajeti ya sasa 2017/18 TAMISEMI imetenga bajeti ya elfu moja kwa kila mtoto na kuweka jumla ya Shilingi bilioni 1 “
Aidha alisema ni wajibu wa kila Mkuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha wanasimamia utekelezaji wa afua zilizoanishwa katika mpango jumuishi wa utekelezaji wa masuala ya lishe ili kuboresha afya na kuendeleza agenda ya lishe katika kuleta maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
Aliongeza kuwa Taifa linahitaji watu wenye afya bora ili waweze kuchangia katika kuleta maendeleo nchini , mpango huu jumuishi wa lishe 2016/17- 2020/2021 una lengo la kutokomeza utapia mlo na boresha afya ya mtoto hivyo ni wito wa kila mdau wa afya kuhahakisha anasimamia kikamilifu utekelezaji wa mpango huu.
Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kasim Majaliwa alisema kuwa Serikali imejipanga vya kutosha katika kutokomeza utapia mlo nchini hivyo aliwataka wadau kutoa elimu sahihi ya lishe na kulipa kipaumbele suala zima la lishe kwa kubuni sera na mikakati bora ya kilimo na lishe.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Chakula na Lishe Tanzania ( TFNC) Bi. Joseline Kaganda alisema kuwa ili kutokomeza utapia mlo nchini lazima kuwepo na mpango thabiti wa kupambana na chanagamoto hii pamoja na ushirikiano kati ya Serikali na wadau wa lishe.
Naye Mkurugenzi wa USAID na mwakilishi wa Msukumo mpya katika masuala ya lishe (SUN-NETWORK) Bw. Andrew Karas amesema kuwa ushirikishwaji wa wananchi ,wadau na Serikali ni muhimu mno katika kutokomeza utapia mlo Tanzania hivyo ni lazima kuimarisha mahusiano na mifumo iliyopo ili kufikisha huduma kwenye maeneo yaliyo na upungufu.
Mkutano wa nne wa wadau wa sekta ya lishe katika kufanya mapitio ya mpango jumuishi wa lishe 2016/17- 2020/2021 utakaodumu kwa siku tatu katika ukumbi wa mikutano Hazina Mjini Dodoma umehudhuriwa na Maafisa lishe wa Mikoa na Wilaya nchini,Asasi na mashirika ya kiraia yanayotekeleza afua za lishe,sekta binafsi na Wizara mtambuka pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo nchini kwa siku tatu .
Naibu Waziri wa TAMISEMI Mh. Profesa Seleman Jafo akizungumza kwenye wa mkutano wa nne wa wadau wa sekta ya lishe katika kufanya mapitio ya mpango jumuishi wa lishe 2016/17- 2020/2021 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano Hazina Mjini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kasim Majaliwa akimkabidhi Naibu Waziri wa TAMISEMI Mh. Profesa Seleman Jafo mpango mpango jumuishi wa lishe 2016/17- 2020/2021 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano Hazina Mjini Dodoma.
Hivyo makala TAMISEMI YATENGA BILIONI MOJA
yaani makala yote TAMISEMI YATENGA BILIONI MOJA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TAMISEMI YATENGA BILIONI MOJA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/tamisemi-yatenga-bilioni-moja.html
0 Response to "TAMISEMI YATENGA BILIONI MOJA"
Post a Comment