title : SSRA Yatakiwa kusimamia Michango ya Wanachama
kiungo : SSRA Yatakiwa kusimamia Michango ya Wanachama
SSRA Yatakiwa kusimamia Michango ya Wanachama
Na. Zawadi Msalla.
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mh. Alli Karume ameitaka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) kusimamia kwa ukaribu michango ya Wanachama kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ili itumike kwa malengo yaliyokusudiwa kwa mujibu wa Sheria zilizoanzisha mifuko hiyo.
Wito huo umetolewa jana mjini Kigoma na Waziri Karume alipotembelea banda la SSRA kwenye maonesho ya wiki ya Bahari duniani yanayoendelea kwenye viwanja vya shule ya msingi Mlole Mkoani humo.
Waziri Karume alisema SSRA inawajibu mkubwa wa kumlinda mwanachama wake ili kuhakikisha hapati matatizo pale anapotakiwa kupata mafao yake.Pia alisisitiza kuwa Itakuwa ni jambo la kuumiza sana inapotokea mwanachama mwenye matumaini ya kupata mafao yake atakapoambiwa mfuko umefilisika na hivyo mafao anayoyatarajia hawezi kuyapata.
Aidha Mhe. Karume aliipongeza SSRA kwa elimu wanayoendelea kuitoa kwa jamii juu ya umuhimu wa kujiunga na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na jinsi wanavyo simamia maboresho mbalimbali yanayoendelea katika sekta hiyo.
Hata hivyo alisema bado SSRA inawajibu mkubwa wa kutoa elimu kwa jamii ili kushawishi wananchi kuona umuhimu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwani wapo wananchi wengi wasio fahamu umuhimu wa mifuko hiyo na wengi wao hupata shida inapofikia kipindi cha uzeeni.
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Alli Karume akipata maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na SSRA kutoka kwa Afisa Uhusiano wa Mamlaka Bw. Sabato Kosuri alipotembelea banda hilo wakati wa maadhimisho ya siku ya Bahari Duniani yaliyofanyika mkoani Kigoma.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala SSRA Yatakiwa kusimamia Michango ya Wanachama
yaani makala yote SSRA Yatakiwa kusimamia Michango ya Wanachama Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SSRA Yatakiwa kusimamia Michango ya Wanachama mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/ssra-yatakiwa-kusimamia-michango-ya.html
0 Response to "SSRA Yatakiwa kusimamia Michango ya Wanachama"
Post a Comment