SIKU YA MTINDIO WA UBONGO KITAIFA KUFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM.

SIKU YA MTINDIO WA UBONGO KITAIFA KUFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SIKU YA MTINDIO WA UBONGO KITAIFA KUFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SIKU YA MTINDIO WA UBONGO KITAIFA KUFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM.
kiungo : SIKU YA MTINDIO WA UBONGO KITAIFA KUFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM.

soma pia


SIKU YA MTINDIO WA UBONGO KITAIFA KUFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM.


Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO. 

Chama cha Wazazi na Watoto wenye Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo,Akili na Viungo Tanzania (CHAWAUMAVITA) kitafanya maadhimisho ya siku ya mtindio wa ubongo duniani kwa lengo la kuipa jamii uelewa juu ya changamoto wanazozipata watoto wenye matatizo hayo na kuwaleta pamoja familia zinazolea watoto hao ili wabadilishane uzoefu.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na mwenyekiti wa chama hicho, Hilali Said alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho hayo.

“Kwa kawaida Siku ya Mtindio wa Ubongo duniani huadhimishwa kila Jumatano ya kwanza ya mwezi Oktoba lakini kwa mwaka huu itaadhimishwa tarehe 6, ambapo yanategemewa kufanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mjimwema vilivyopo wilaya ya Kigamboni na tunategemea mgeni rasmi wa maadhimisho hayo atakuwa Mkuu wa Wilaya hiyo”, alisema Said.

Said ameongeza kuwa nchi mbalimbali Duniani huadhimisha siku hiyo kwa kutoa elimu ya ulemavu wa aina hiyo kwa wananchi ili kupunguza athari zinazojitokeza kwa wazazi na watoto wenyewe pamoja na kuwasaidia wanachama kutetea na kupata haki zao kwa mujibu wa sheria.
Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi wa Watoto Wenye Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo, Akili na Viungo Tanzania (CHAMAUMAVITA) Bw. Hilally Said (katikati), akisisitiza jambo mbele ya Waaandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya maadhimisho ya Watoto wenye Mtindio wa Ubongo yatakayofanyika tarehe 6 oktoba mwaka huu leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu wa CHAMAUMAVITA Taifa, Bi. Mwanahamis Hussein, na Mweka Hazina wa CHAMAUMAVITA Taifa Bi. Jane Kim.
Katibu wa Chama cha Wazazi wa Watoto Wenye Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo, Akili na Viungo Tanzania (CHAMAUMAVITA) Taifa, Bi. Mwanahamis Hussein (katikati) akizungumza mbele ya waandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya maadhimisho ya watoto wenye Mtindio wa Ubongo yatakayofanyika tarehe 6, Oktoba mwaka huu leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa CHAMAUMAVITA Bw. Hilali Said na Mweka Hazina wa CHAMAUMAVITA Taifa Bi. Jane Kim.
Mweka Hazina wa Chama cha Wazazi wa Watoto Wenye Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo, Akili na Viungo Tanzania (CHAMAUMAVITA), Bi. Jane Kim akielezea maadhimisho ya Watoto wenye Mtindio wa Ubongo yatakayofanyika tarehe 6, Oktoba mwaka huu mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani, Kushoto ni Mwenyekiti wa CHAMAUMAVITA Bw. Hilali Said. Picha zote na Thobias Robert, MAELEZO.




Hivyo makala SIKU YA MTINDIO WA UBONGO KITAIFA KUFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM.

yaani makala yote SIKU YA MTINDIO WA UBONGO KITAIFA KUFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SIKU YA MTINDIO WA UBONGO KITAIFA KUFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/siku-ya-mtindio-wa-ubongo-kitaifa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SIKU YA MTINDIO WA UBONGO KITAIFA KUFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM."

Post a Comment