title : SERIKALI YAIPONGEZA COSTECH-OFAB KWA KUANDAA TUZO ZA WAANDISHI WA HABARI ZA SAYANSI 2017
kiungo : SERIKALI YAIPONGEZA COSTECH-OFAB KWA KUANDAA TUZO ZA WAANDISHI WA HABARI ZA SAYANSI 2017
SERIKALI YAIPONGEZA COSTECH-OFAB KWA KUANDAA TUZO ZA WAANDISHI WA HABARI ZA SAYANSI 2017
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amewataka waandishi wa habari nchini kutumia taaluma zao kuelimisha jamii kuhusu habari za sayansi na teknolojia ili kuleta maendeleo nchini.
Akizungumza wakati wa utoaji tuzo za umahiri katika uandishi wa habari za Sayansi zilizoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknlojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknojia (OFAB), Waziri Ndalichako alisema tuzo hizo iwe ni chachu za kuandika habari za sayansi kwa undani ili kuwajengea uelewa wananchi wa.kawaida.
Alisema ufundi wa waandishi katika.kuandika habari za sayansi utasaidia kutangaza ubunifu na kuongeza tija thamani katika teknolojia mbalimbali."Wananchi wanahitaji teknolojia za kisasa katika kurahisisha utendaji kazi hivyo uandishi wenu utasaidia kuinua sekta ya kilimo na mifugo ambayo ndio kundi.muhimu katika jamii hasa katika kuelekea uchumi wa viwanda,"alisema Ndalichako.
Aliwataka Costech na taasisi nyingine kuendelea kushirikiana na wanahabari kuelimisha jamii katika masuala ya sayansi.Ndalichako alipongeza COSTECH na OFAB kwa kuandaa tuzo hizo kwani zitaongeza mori kwa wanahabari wa kuandika habari za sayansi.
Akielezea ushiriki wa.waandishi katika shindano hilo lililoanza Januari hadi Agosti mwaka hii, Mkurugenzi Mkuu wa COTECH, Dk.Hassan Mshinda alisema, shindano hilo hapa nchini sasa ni mara ya tisa kufanyika na kwa upande wa Afrika ni la kumi.
Mwandishi wa Habari wa gazeti la Guardian, Gerald Kitabu akipeana mkono na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia , Profesa Joyce Ndalichako baada ya kukabidhiwa tuzo ya mshindi wa kwanza kwenye kuandika na kuelimisha umma kuhusu matumizi ya sayansi, Teknolojia na ubunifu hususani Bioteknolojia katika kuendeleza kilimo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk. Hassan Mshinda
Waziri Ndalichako akihutubia katika hafla hiyo.
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Jim Yonaz akitoa hutuba katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa COTECH, Dk.Hassan Mshinda akizungumzia tuzo hizo
Hivyo makala SERIKALI YAIPONGEZA COSTECH-OFAB KWA KUANDAA TUZO ZA WAANDISHI WA HABARI ZA SAYANSI 2017
yaani makala yote SERIKALI YAIPONGEZA COSTECH-OFAB KWA KUANDAA TUZO ZA WAANDISHI WA HABARI ZA SAYANSI 2017 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAIPONGEZA COSTECH-OFAB KWA KUANDAA TUZO ZA WAANDISHI WA HABARI ZA SAYANSI 2017 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/serikali-yaipongeza-costech-ofab-kwa.html
0 Response to "SERIKALI YAIPONGEZA COSTECH-OFAB KWA KUANDAA TUZO ZA WAANDISHI WA HABARI ZA SAYANSI 2017"
Post a Comment