title : SERIKALI ITAHAKIKISHA MIRADI YA UMEME, MBAGALA, KURASINI NA KIGAMBONI INAKAMILIKA-DKT. KALEMANI
kiungo : SERIKALI ITAHAKIKISHA MIRADI YA UMEME, MBAGALA, KURASINI NA KIGAMBONI INAKAMILIKA-DKT. KALEMANI
SERIKALI ITAHAKIKISHA MIRADI YA UMEME, MBAGALA, KURASINI NA KIGAMBONI INAKAMILIKA-DKT. KALEMANI
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
SERIKALI kupitia Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), imeahidi kusimamia miradi ya umeme Kituo cha Tipper-Kigamboni, Mbagala na Kurasini ili kuhakikisha inakamilika kwa haraka na kwa wakati na hatimaye wananchi wa maeneo hayo wanaondokana na adha ya kukatika kwa umeme mara kwa mara.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, mwishoni mwa ziara yake ya kufuatilia uboreshaji wa vituo vya kupoza na kusambaza umeme pamoja na ujenzi wa kituo kipya cha kufua na kusambaza umeme huko Kimbiji wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam Septemba 18, 2017.
Waziri pia amekagua ujenzi wa mradi wa maendeleo ya upanuzi na upatikanaji nishati (TEDAP), wa kusafirisha umeme wa 132kv ulioko Gongolamboto nje kidogo ya jiji.
“Wananchi wanataka umeme, hawahitaji kujua nguzo za umeme zimepatikana wapi, au upembuzi yakinifu utakamilika lini, nimeagiza baada ya siku tano kuanzia leo (Septemba 18), fanyeni kazi usiku na mchana walau vituo viwili vya kupoza na kusambaza umeme viwe vimekamilika ili wananchi wa Mbagala na Kigamboni wapate umeme wa kutosha.” Alisema Dkt.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, (wakwanza kulia), Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka, (wakwanza kushoto), na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo anayeshughulikia Miradi, Mhandisi Khalid James, (watatu kushoto), wakimsikiliza Meneja Mradi wa TEDAP, Mhandisi Emmanuel Manirabona, (aliyenyoosha mkono), wakati Naibu Waziri na uongpozi wa TANESCO, ulipotembelea mradi wa TEDAP wa Gongolamboto jijini Dar es Salaam, Septemba 18, 2017. Mradi huo unahusu upanuzi na uendelezaji wa mradi wa kusafirisha umeme wa 132kv.
Mbunge wa Kigamboni Mhe. Dkt. Faustine Ndungulile, (kushoto), akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani ambaye alifuatana naye kwenye ziara hiyo.
Sakafu ya kufungia transfoma mpya ya umeme wa 15mva kituo cha Tipper-Kigamboni, ikijengwa Septemba 18, 2017
Hivyo makala SERIKALI ITAHAKIKISHA MIRADI YA UMEME, MBAGALA, KURASINI NA KIGAMBONI INAKAMILIKA-DKT. KALEMANI
yaani makala yote SERIKALI ITAHAKIKISHA MIRADI YA UMEME, MBAGALA, KURASINI NA KIGAMBONI INAKAMILIKA-DKT. KALEMANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI ITAHAKIKISHA MIRADI YA UMEME, MBAGALA, KURASINI NA KIGAMBONI INAKAMILIKA-DKT. KALEMANI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/serikali-itahakikisha-miradi-ya-umeme.html
0 Response to "SERIKALI ITAHAKIKISHA MIRADI YA UMEME, MBAGALA, KURASINI NA KIGAMBONI INAKAMILIKA-DKT. KALEMANI"
Post a Comment