Ni JKU na Miembeni City Kesho Ngao ya Jamii.

Ni JKU na Miembeni City Kesho Ngao ya Jamii. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Ni JKU na Miembeni City Kesho Ngao ya Jamii., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Ni JKU na Miembeni City Kesho Ngao ya Jamii.
kiungo : Ni JKU na Miembeni City Kesho Ngao ya Jamii.

soma pia


Ni JKU na Miembeni City Kesho Ngao ya Jamii.

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
PAZIA la msimu ujao wa Ligi Kuu Soka Visiwani Zanzibar linatarajiwa kufunguliwa rasmi kesho Jumanne Septemba 19 kwa mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya JKU na Miembeni City, utakaofanyika kwenye Uwanja wa Amaan, Mjini Unguja majira ya Saa 10 za jioni.

Kuelekea mchezo huo tumezungumza na katibu wa timu ya JKU Saadu Ujudi ambapo amesema hawana wasi wasi wowote kwenye mchezo huo huku akiamini watatwaa Ngao hiyo.

“Sisi JKU hatuna hofu juu ya Miembeni City mimi niwaombe Mashabiki wafike kwa wingi kuja kuangalia wenyewe mchezo huo”. Alisema Ujudi.

Nae Ali Khamis ambae ni afisa habari wa Miembeni City amesema msimu huu wamekuja kufanya mapinduzi kwa timu za vikosi ambazo zinaonekana kutawala kwa muda mrefu soka la Zanzibar.

“Miembeni City tumekuja kufanya mapinduzi kwa timu za vikosi, na tutaanza kuwaonyesha kwenye mchezo huo wa Ngao”. Alisema Khamis.

Ligi kuu soka Visiwani Zanzibar inatarajiwa kuanza Oktoba 3, mwaka huu, kwa timu mbalimbali kuonyeshana kazi kwenye uwanja wa Amaan Mjini Unguja na Gombani Kisiwani Pemba.

JKU ndio wanaoshikilia ubingwa wa ligi hiyo, inayoshirikisha timu 28 kwa Zanzibar nzima ambapo kila kanda inajumla ya timu 14.


Hivyo makala Ni JKU na Miembeni City Kesho Ngao ya Jamii.

yaani makala yote Ni JKU na Miembeni City Kesho Ngao ya Jamii. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Ni JKU na Miembeni City Kesho Ngao ya Jamii. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/ni-jku-na-miembeni-city-kesho-ngao-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Ni JKU na Miembeni City Kesho Ngao ya Jamii."

Post a Comment