title : MAWASILIANO YAONGEZA KASI YA UKUSANYAJI WA MAPATO YA SERIKALI
kiungo : MAWASILIANO YAONGEZA KASI YA UKUSANYAJI WA MAPATO YA SERIKALI
MAWASILIANO YAONGEZA KASI YA UKUSANYAJI WA MAPATO YA SERIKALI
Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli imesisitiza kwa taasisi za Serikali, sekta binafsi na wananchi kwa ujumla kulipa kodi kwa wakati ili nchi iweze kuongeza mapato yake kwa lengo la kukuza uchumi, kujenga miundombinu ya barabara, reli, bandari, mawasiliano, kuboresha utoaji wa huduma za kijamii na kuweza kuwatumika wananchi.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Prof. Norman Sigalla wakati wa ziara ya Kamati yake ya kukagua ujenzi wa minara, ufikishaji na upatikanaji wa huduma za mawasiliano vijijini na kwenye maeneo yasiyo na mvuto wa kibishara kwenye mikoa ya kanda ya ziwa ya Mwanza na Mara ambapo Serikali imetoa ruzuku kwa makampuni ya simu za mkononi ili ziweze kutoa huduma za mawasiliano kwa wananchi kupitia Mfuko wa Mawasiliao kwa Wote (UCSAF) ulio chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Ameongeza kuwa Kamati yake inasimamia sekta ya miundombinu yote nchini ikiwa ni pamoja na miundombinu ya mawasiliano ambayo inategemewa na Serikali katika kukuza uchumi na kuiwezesha nchi yetu kufikia uchumi wa kati na kuwa nchi ya viwanda. Prof. Norman Sigalla King amesema kuwa miundombinu na huduma za mawasiliano ni moja ya nguzo kuu za ukuaji wa uchumi, inachochea maendeleo ya taifa letu na kuiwezesha Serikali kuhudumia wananchi wake kwa haraka, wakati, kwa ufanisi na kupunguza gharama za Serikali kuwahudumia wananchi na kuokoa muda. “Serikali imepeleka fedha nyingi kwa ajili ya miundombinu mbalimbali ya nchi yetu kupitia Wizara hii kwenye bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha wa 2017/2018 ili nchi iweze kusonga mbele”, amesema Prof. Norman Sigalla King.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Prof. Norman Sigalla King akisisitiza jambo wakati wa ziara ya Kamati ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mnara wa TTCL kwenye kijiji cha Sanga Itinje kilichopo Kata ya Itinje wilaya ya Meatu mkoani Simiyu. Kushoto kwa Mwenyekiti ni Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Eng. Peter Ulanga.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bwana John Mongella akiongea kuhusu mchango wa mifumo ya mawasiliano katika kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato ya Serikali mbele ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu na watendaji wa kampuni za simu wa mkoani Mwanza (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kukagua ujenzi wa minara, ufikishaji na upatikanaji wa huduma za mawasiliano vijijini mkoani Mwanza. Aliyeketi ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Prof. Norman Sigalla King.
Meneja wa TTCL mkoa wa Shinyanga Bwana Abdallah Lugage akitoa taarifa kwa Kamati ya Bunge ya Miundombinu kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mnara wa kampuni hiyo kwenye kijiji cha Sanga Intinje kilichopo kata ya Intinje wilaya ya Meatu mkoani Simiyu. Wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Prof. Norman Sigalla King.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, watendaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, wafanyakazi wa TTCL na wanakijiji wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mnara wa kampuni hiyo kwenye kijiji cha Sanga Intinje kata ya Intinje iliyopo wilaya ya Meatu mkoani Simiyu.
Hivyo makala MAWASILIANO YAONGEZA KASI YA UKUSANYAJI WA MAPATO YA SERIKALI
yaani makala yote MAWASILIANO YAONGEZA KASI YA UKUSANYAJI WA MAPATO YA SERIKALI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAWASILIANO YAONGEZA KASI YA UKUSANYAJI WA MAPATO YA SERIKALI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/mawasiliano-yaongeza-kasi-ya-ukusanyaji.html
0 Response to "MAWASILIANO YAONGEZA KASI YA UKUSANYAJI WA MAPATO YA SERIKALI"
Post a Comment