title : Makamu wa Rais, Bi Samia Azinduwa Tamasha la Jinsia 2017
kiungo : Makamu wa Rais, Bi Samia Azinduwa Tamasha la Jinsia 2017
Makamu wa Rais, Bi Samia Azinduwa Tamasha la Jinsia 2017
MAKAMU wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu leo amezinduwa rasmi Tamasha la Jinsia Tanzania mwaka 2017. Uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam, ambapo mbali na uzinduzi huo ameongoza zoezi la kutoa tuzo kwa baadhi ya akinamama waliofanya vizuri na kutoa mchango katika maendeleo ya wanawake.
Akizungumza kabla ya uzinduziwa tamasha hilo, Makamu wa Rais, Bi. Samia Suluhu aliipongeza TGNP kwa harakati zake za kuiunga mkono na kuikosoa serikali pale wanapoona imekwenda tofauti.
Alisema kitendo cha kukemea na kutoa mapendekezo na suluhisho sehemu ambayo wanaamini serikali haijafanya vizuri ni kitendo cha kiungwana na kinachochea maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Alisema hatua tuliofikia sasa si ya kulaumiana bali kushirikiana katika kuliletea taifa maendeleo. Alisema Serikali ya Jamhuri ya Tanzania inatambua umuhimu wa kuzingatia usawa wa jinsia katika kuchangia na kuendeleza maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Alisema Serikali tangua uhuru hatua kwa hatua imekuwa ikizingatia utungwaji wa sheria na kanuni rafiki zinazosimamia usawa wa jinsia.
Aliongeza Tanzania kama mwanachama wa UN na AU imekuwa imeridhia mikataba na itifaki na makubaliano mbalimbali ya kimataifa na kikanda kuhusiana na usawa wa jinsia na uwezeshaji wanawake, utekelezaji wa makubaliano ya uringo wa Beingin, Malengo ya Maendeleo Endelevu pamoja na mkataba wa kupinga aina zote za ubaguzi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Vicensia Shule aliwataja na kuwapongeza wanawake waliofanya vizuri maeneo mbalimbali ambapo Makamu wa Rais alikabidhi tuzo kwa wakinamama hao. Miongoni waliopokea tuzo ni pamoja na Makamu wa Rais wa Tanzania, Bi. Suluhu, aliyekabidhiwa tuzo yake na Mwenyekiti wa bodi.
Wengine ni pamoja na Spika mstaafu wa Bunge la Tanzania, Anna Makinda, Mbunge wa Bunda Mjini, Estar Bulaya, Mama Getrude Mongela, Dk. Ester Mwaikambo, na Msanii Fatma Baraka (Bi. Kidude) kwa jitihada walizozionesha katika uongozi na wote walipewa tuzo.
Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu akicheza na wasanii na wageni waalikwa.
Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu (kushoto) akikabidhi tuzo mmoja wa wanachama waanzilishi wa TGNP, Bi. Marjorie Mbilinyi (kulia)
Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu (kushoto) akikabidhi tuzo kwa Zipora Shekilango (kulia) kwenye uzinduzi rasmi wa Tamasha la Jinsia Tanzania la mwaka 2017.
Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu (kushoto) akikabidhi tuzo mmoja wa wanachama waanzilishi wa TGNP, Bi. Marry Lusimbi (kulia) kwenye uzinduzi rasmi wa Tamasha la Jinsia Tanzania la mwaka 2017.width="500"]
Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu (kushoto) akikabidhi tuzo mwakilishi wa halmashauri ya Kishapu kwa kufanikiwa kuwawezesha akinamama.
Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu (kushoto) akikabidhi tuzo mwakilishi wa halmashauri Kisarawe.[/caption]
Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu (kushoto) akikabidhi daktari wa kwanza mwanamke Tanzania, Dk. Ester Mwaikambo (kulia)
Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu akitembelea miradi mbalimbali na shughuli za akinamama wanaharakati ngazi ya jamii za kujikwamua.
Hivyo makala Makamu wa Rais, Bi Samia Azinduwa Tamasha la Jinsia 2017
yaani makala yote Makamu wa Rais, Bi Samia Azinduwa Tamasha la Jinsia 2017 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Makamu wa Rais, Bi Samia Azinduwa Tamasha la Jinsia 2017 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/makamu-wa-rais-bi-samia-azinduwa.html
0 Response to "Makamu wa Rais, Bi Samia Azinduwa Tamasha la Jinsia 2017"
Post a Comment