title : KAMATI YA BUNGE YA HAKI, MAADILI NA MADARAKA YAMUHOJI ZITTO KABWE
kiungo : KAMATI YA BUNGE YA HAKI, MAADILI NA MADARAKA YAMUHOJI ZITTO KABWE
KAMATI YA BUNGE YA HAKI, MAADILI NA MADARAKA YAMUHOJI ZITTO KABWE
Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, leo imemuhoji Mbunge Kigoma Mjini Zitto kufuatia agizo la Mheshimiwa Spika la kumtaka Mbunge huyo ahojiwe kutokana na kauli mbalimbali alizozitoa za kulidharau Bunge.
Zitto alifika mbele ya Kamati hiyo majira ya saa 9 alasiri na kuhojiwa kwa takribani saa tatu.
Akizungumzia kikao hicho, Mwenyekiti wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Mhe. Kapteni Mstaafu George Mkuchika alisema Kamati imesikiliza maelezo ya Mhe. Zitto kuhusiana na tuhuma ambazo zilikuwa zinamkabili.
“Kamati imemhoji Mheshimiwa Zitto amejibu maswali yote aliyotakiwa kuyajibu, Kamati imemaliza kazi yake na kwa mujibu wa utaratibu uliopo ikimaliza kazi inaanda Ripoti na kuipeleka kwa Mheshimiwa Spika,” ,” alisema.
Akizungumzia sababu za Zitto kupelekwa mbele ya Kamati hiyo chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisli alisema kwa mujibu wa Sheria ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge mtu anayeitwa mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge hupelekewa Hati ya Kuitwa na Katibu wa Bunge.
“Kutokana na kwamba hakufika na hakukuwa mawasiliano yoyote, Sheria inaruhusu Mhe. Spika kutoa Hati ya kukamatwa na kuletwa kwenye kikao cha Kamati,” alisema.
Alisema Mhe. Zitto alipewa Hati ya kuitwa Septemba 13 kwa ajili ya kufika mbele ya Kamati kesho yake Septemba 14 lakini hakufika na hakutoa taarifa ndio maana akapelekwa pale chini ya ulinzi wa polisi.
Septemba 12, mwaka huu, Mhe. Spika Job Ndugai aliagiza Mbunge huyo kufika mbele ya kamati hiyo kwa ajili ya kuhojiwa kuhusiana na kauli zake alizozitoa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Mhimili wa Bunge umewekwa mfukoni na Serikali na kwamba Bunge lilikosea kushughulikia Taarifa za Kamati kuhusu Almasi na Tanzanite.
Hivyo makala KAMATI YA BUNGE YA HAKI, MAADILI NA MADARAKA YAMUHOJI ZITTO KABWE
yaani makala yote KAMATI YA BUNGE YA HAKI, MAADILI NA MADARAKA YAMUHOJI ZITTO KABWE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KAMATI YA BUNGE YA HAKI, MAADILI NA MADARAKA YAMUHOJI ZITTO KABWE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/kamati-ya-bunge-ya-haki-maadili-na.html
0 Response to "KAMATI YA BUNGE YA HAKI, MAADILI NA MADARAKA YAMUHOJI ZITTO KABWE"
Post a Comment