title : Ecobank yazindua njia salama ya malipo kwa mtandao
kiungo : Ecobank yazindua njia salama ya malipo kwa mtandao
Ecobank yazindua njia salama ya malipo kwa mtandao
Ecobank yaja na suluhisho la kufanya malipo salama kwa njia mtandao kupitia MASTERPASS na MVISA .
Ecobank katika kuendeleza dhamira yake ya kutoa huduma bora na kuwa suluhisho kwenye sekta ya biashara ya huduma za kibenki hapa nchini leo imezindua applikesheni ya simu za mkononi itakayojulikana kama Ecobank Mobile App – MASTERPASS NA MVISA ili kusaidia wafanyabiashara na watoa huduma mbalimbali kufanya Malipo kwa njia rahisi na kwa usalama zaidi mahali popote.
Mtanzania yeyote ataweza kutumia teknolojia hii ya mpya ya MASTERPASS QR na MVISA kulipia gharama mbali mbali kwa kutumia simu zao za mkononi kwa kupitisha Quick Response (QR) kwa wauzaji mbalimbali wa bidhaa au watoa huduma ndani na nje ya nchi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania Bi, Mwanahiba Mzee alisema “applikesheni ya Ecobank Mobile App ilizinduliwa Februari mwaka huu lakini kwa sasa imeboreshwa zaidi ili wateja wa Ecobank na wale wasio wateja wa bank hii waweze kutumia applikesheni hii duniani kote”.
‘Applikesheni ya Ecobank Mobile App ni njia rahisi ya kujipatia huduma za kibenki ndani ya nchi 33 ambazo Benki yetu inafanya biashara lakini pia unaweza kuitumia ukiwa kokote duniani. Wateja wanaweza kupakua applikesheni Ecobank Mobile App na papo hapo kujifungulia akaunti ya Ecobank kwa njia ya mtandao na kuanza kupata huduma za kibenki kama vile kufanya malipo au kuhamisha fedha bila kutembelea tawi lolote la Benki”, alisema Bi Mzee.
“Tunayo furaha kwamba applikesheni yetu ni sulushisho la huduma za haraka za kibenki kupitia mtandao wa simu za mkononi na bado inaendea kuboreshwa zaidi na zaidi na sasa tunatumia teknolojia ya Masterpass QR na Mvisa kwa kufanya malipo mbali mbali, aliongeza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ,Ecobank Tanzania, Mwanaiba Mzee, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa Uzinduzi huduma ya Malipo kwa njia ya Mtandao, inayayojulikana kama MasterPass na MVISA .Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki hiyo, Respige Kimati na Mkuu wa Kitengo cha wateja wa Reja reja, Ndabu Sware (kushoto).
Mkuu wa Kitengo cha wateja wa Reja Reja wa Ecobank Ndabu Lilian Sware (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa Uzinduzi huduma ya Malipo kwa njia ya Mtandao, inayayojulikana kama MasterPass na MVISA. Kati kati Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Mwanaiba Mzee na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki hiyo, Respige Kimati.
Baadhi ya wafanyakazi wa Ecobank Tanzania wakifuatilia kwa umakini wa Uzinduzi wa huduma ya Malipo kwa njia ya Mtandao, inayayojulikana kama MasterPass na MVISA. Ecobank Tanzania inakuwa Benki ya kwanza hapa Tanzania kuzindua huduma ya Mobile App ambayo inakuwa ni suluhisho kwa huduma za kifedha.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Ecobank yazindua njia salama ya malipo kwa mtandao
yaani makala yote Ecobank yazindua njia salama ya malipo kwa mtandao Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Ecobank yazindua njia salama ya malipo kwa mtandao mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/ecobank-yazindua-njia-salama-ya-malipo.html
0 Response to "Ecobank yazindua njia salama ya malipo kwa mtandao"
Post a Comment