Dkt. Mwakyembe aongoza Mamia kuaga Mwili wa Muhingo Rweyemamu

Dkt. Mwakyembe aongoza Mamia kuaga Mwili wa Muhingo Rweyemamu - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Dkt. Mwakyembe aongoza Mamia kuaga Mwili wa Muhingo Rweyemamu, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Dkt. Mwakyembe aongoza Mamia kuaga Mwili wa Muhingo Rweyemamu
kiungo : Dkt. Mwakyembe aongoza Mamia kuaga Mwili wa Muhingo Rweyemamu

soma pia


Dkt. Mwakyembe aongoza Mamia kuaga Mwili wa Muhingo Rweyemamu

 Mwambawahabari
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akitoa salaamu za pole za Serikali na Wizara yake  leo Jijini Dar es Salaam wakati wa kuaga mwili wa Mkuu wa Wilaya mstaafu na Mwanahabari Marehemu Muhingo Rweyemamu aliefariki Septemba 2 mwaka huu katika hospitali ya Agha Khan.

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akitoa heshima za mwisho leo Jijini Dar es Salaam  kwa mwili  wa Mkuu wa Wilaya mstaafu na Mwanahabari Marehemu Muhingo Rweyemamu  aliefariki Septemba 2 mwaka huu katika hospitali ya Agha Khan.

 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda  akitoa heshima za mwisho leo Jijini Dar es Salaam  kwa mwili  wa Mkuu wa Wilaya mstaafu na Mwanahabari Marehemu Muhingo Rweyemamu  aliefariki Septemba 2 mwaka huu katika hospitali ya Agha Khan
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bibi Sophia Mjema akitoa heshima za mwisho leo Jijini Dar es Salaam  kwa mwili  wa Mkuu wa Wilaya mstaafu na Mwanahabari Marehemu Muhingo Rweyemamu  aliefariki Septemba 2 mwaka huu katika hospitali ya Agha Khan.

 Baadhi ya waombolezaji wakifuatilia tukio la kuaga mwili wa Mkuu wa Wilaya mstaafu na Mwanahabari Marehemu Muhingo Rweyemamu  aliefariki Septemba 2 mwaka huu katika hospitali ya Agha Khan.

  Mkuu wa Wilaya ya Handeni Bw.Godwin Gondwe akizungumza wakati wa kuaga mwili wa mkuu wa wilaya mstaafu na Mwanahabari Marehemu Muhingo Rweyemamu aliefariki Septemba 2 mwaka huu katika hospitali ya Agha Khan.


Mtoto wa marehemu Muhingo Rweyemamu  Bw. Emmanuel Muhingo akisoma wasifu wa baba yake  aliefariki Septemba 2 mwaka huu katika hospitali ya Agha Khan wakati wa kuagwa leo Jijini Dar es Salaam .
Na Shamimu Nyaki-WHUSM
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Dkt. Harrison Mwakyembe ameongoza mamia ya waombolezaji kuaga mwili wa Mkuu wa Wilaya mstaafu na Mwanahabari,  marehemu Muhingo Rweyemamu  aliyefariki Septemba 2 mwaka huu katika hospitali ya Agha Khan.
Akitoa salamu za pole kwa niaba ya Serikali  na Wizara yake leo Jijini Dar es Salaam, Mhe. Mwakyembe amemuelezea marehemu  Rweyemamu kuwa alikua mtumishi mzuri katika Serikali hasa katika wadhifa wake wa Ukuu wa Wilaya na mara zote alihakikisha Wananchi anaowaongoza wanakuwa wachapakazi kwa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
“Serikali inatoa pole sana kwa familia na wanatasnia ya habari kwani marehemu Rweyemamu ameacha pengo kubwa kwa familia yake na wanahabari kutokana na uhodari wake katika uandishi lakini pia Serikali inakumbuka uchapakazi wake alipokua Serikalini. Tunaomba Mungu awape faraja na uvumilivu wafiwa wote”. Alisema Mhe. Mwakyembe.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Godwin Gondwe amemuelezea marehemu kuwa alikuwa mchapakazi hodari wakati alipokuwa Mkuu wa Wilaya hiyo na Wananchi wa Handeni watamkumbuka katika jitihada zake za kuhimiza watoto wa kike kupenda shule ambapo alianzisha kampeni iliyoitwa “niache nisome” lengo likiwa ni kuelimisha umuhimu wa elimu kwa mtoto wa kike.
“Wananchi wa handeni wamesikitishwa sana na kifo hiki kwani wanakumbuka uhodari wake katika kuwatumikia alipokuwa mkuu wa Wilaya yao hasa juhudi zake za kuhimiza jamii kupeleka watoto shule kwa manufaa yao ya baadae”. Alisema Mhe. Gondwe”.
Naye mwakilishi kutoka vyombo vya habari Bw. Absolum Kibanda amesema kuwa marehemu alikuwa mwalimu na mshauri mzuri katika tasnia ya habari na alikuwa anaipenda kazi yake na kufanya  waandishi wengi kuiga na kujifunza kutoka kwake uandishi wa habari za uchunguzi na makala.
Marehemu Muhigo Ryeyemamu amewahi kufanya kazi katika magazeti ya mbalimbali hapa nchini ikiwemo Mtanzania, Mwananchi, Rai, The Citizen akitumikia nyadhifa mbalimbali kama mhariri  na mwandishi. Marehemu amezikwa leo katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam na ameacha mke,watoto wanne na mjukuu mmoja.



Hivyo makala Dkt. Mwakyembe aongoza Mamia kuaga Mwili wa Muhingo Rweyemamu

yaani makala yote Dkt. Mwakyembe aongoza Mamia kuaga Mwili wa Muhingo Rweyemamu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Dkt. Mwakyembe aongoza Mamia kuaga Mwili wa Muhingo Rweyemamu mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/dkt-mwakyembe-aongoza-mamia-kuaga-mwili.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Dkt. Mwakyembe aongoza Mamia kuaga Mwili wa Muhingo Rweyemamu"

Post a Comment