title : DC MTATURU AWASIHI VIJANA KUDUMISHA NIDHAMU NA MSHIKAMANO
kiungo : DC MTATURU AWASIHI VIJANA KUDUMISHA NIDHAMU NA MSHIKAMANO
DC MTATURU AWASIHI VIJANA KUDUMISHA NIDHAMU NA MSHIKAMANO
Na Mathias Canal, Singida
Vijana wametakiwa kusimamia misingi ya Nidhamu ndani na nje ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi kwa kuhuisha mshikamano ili kulinda misingi ya Utaifa na uwajibikaji kwani wao ndio nguvukazi ya Taifa na ushindi wa Chama Cha Mapinduzi.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya siasa Wilaya wakati akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Ikungi kwenye mkutano wa uchaguzi wa viongozi wa Jumuiya hiyo katika ukumbi wa shule ya Sekondari Ikungi.
Mhe Mtaturu alisema kuwa Dhana ya Demokrasia ni jambo muhimu linalohitaji kuheshimiwa na kuenziwa ndani ya Chama na Jumuiya zake hivyo kuimarisha nidhamu, mshikamano na upendo ndio silaha pekee itakayoleta heshima ndani ya jumuiya ya vijana wa CCM ili iweze kusonga mbele zaidi na kuwa na mafanikio makubwa katika kuimarisha kipato cha vijana.
Alisema kuwa Nia ya UVCCM ni kujenga na kudumisha haiba njema ya kuendelea kuheshimu misingi ya demorasia ya kweli, yenye kuchunga adabu na kufuata nidhamu, miiko na maadili kwa kila mwanachama anayetaka kutumia haki ya kuchagua au kuchaguliwa.
Hivyo makala DC MTATURU AWASIHI VIJANA KUDUMISHA NIDHAMU NA MSHIKAMANO
yaani makala yote DC MTATURU AWASIHI VIJANA KUDUMISHA NIDHAMU NA MSHIKAMANO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC MTATURU AWASIHI VIJANA KUDUMISHA NIDHAMU NA MSHIKAMANO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/dc-mtaturu-awasihi-vijana-kudumisha.html
0 Response to "DC MTATURU AWASIHI VIJANA KUDUMISHA NIDHAMU NA MSHIKAMANO"
Post a Comment