title : DC KILOLO AWATAKA WAZAZI KUWASOMESHA WATOTO WAO
kiungo : DC KILOLO AWATAKA WAZAZI KUWASOMESHA WATOTO WAO
DC KILOLO AWATAKA WAZAZI KUWASOMESHA WATOTO WAO
Na Fredy Mgunda,Iringa
Wanachi wa kijiji cha mwatasi wamekuwa kikwazo cha wanafunzi kufanya vizuri katika masomo ya shule ya msingi kutokana na wazazi kutowatimizia mahitaji muhimu watoto wao pindi waendepo shule.
Akizungumza na waandishi wa habari waliofika katika shule hiyo mwalimu mkuu wa shule ya msingi mwatasi Seth Mfikwa alisema kuwa wazazi wengi wa kijiji hicho wamekuwa kikwazo cha maendeleo ya wanafunzi kwa kuwakatisha tamaa juu ya umuhimu wa elimu.
“Hapa kijijini wazazi wengi hawapendi watoto wao kwenda kusoma kwa kuwa watakuwa wanapunguza nguvu kazi zao mashambani ndio maana hawawapatii mahitaji muhimu ya kuwasaidia wanafunzi kusoma kwa uhuru” alisema Mfikwa
Mfikwa alimuomba mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah kutafuta wataalam wa saikolojia kuja kuwapa elimu wazazi wa kijiji cha Mwatasi ili kukuza taaluma kwa wanafunzi wa kijiji hicho.
“Ukiangalia hali ya ufaulu wa shule hii sio mzuri kutokana na wazazi kutokujua umuhimu wa elimu lakini tunaendelea kuwaelimisha kidogo kidogo hivyo kwa kuwa mkuu leo umefika kwenye shule yetu tunaomba msaada wako wa kutoa elimu kwa wazazi ili kukuza elimu kwa wanafunzi wa kijiji hiki” alisema Mfikwa.
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdallah akiwa katika ziara ya kuzitembelea shule za msingi za kata ya Bomalang'ombe na kujionea jinsi gani shule hizo zinavyoongozwa na kuzitambua changamoto zinazowakabili walimu,wanafunzi,wanachi na viongozi wanaozizunguka shule hizo lengo likiwa ni kuboresha utoaji wa elimu bora kwa wanafunzi wa wilaya ya kilolo.
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdallah akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Bomalang'ombe.
Hivyo makala DC KILOLO AWATAKA WAZAZI KUWASOMESHA WATOTO WAO
yaani makala yote DC KILOLO AWATAKA WAZAZI KUWASOMESHA WATOTO WAO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC KILOLO AWATAKA WAZAZI KUWASOMESHA WATOTO WAO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/dc-kilolo-awataka-wazazi-kuwasomesha.html
0 Response to "DC KILOLO AWATAKA WAZAZI KUWASOMESHA WATOTO WAO"
Post a Comment