title : BANK OF AFRICA – TANZANIA yazindua program mpya ya kibenki ya “SWAHIBA MOBILE APP”
kiungo : BANK OF AFRICA – TANZANIA yazindua program mpya ya kibenki ya “SWAHIBA MOBILE APP”
BANK OF AFRICA – TANZANIA yazindua program mpya ya kibenki ya “SWAHIBA MOBILE APP”
BANK OF AFRICA – TANZANIA imezindua programu yake mpya ya kibenki inayoitwa "SWAHIBA Mobile" kwenye soko la Tanzania. Huduma hii inakuja kama muendelezo wa programu ya B- Mobile, inayoruhusu watumiaji kufurahia huduma kamili za kibenki kupitia aina yoyote ya simu za mkononi, wakati wowote.
SWAHIBA Mobile App inawapa wateja urahisi wa kutumia huduma za kibenki katika simu kwani inakuja na muonekano mzuri Zaidi na sifa nyingi mpya zinanzowarahisishia wateja kufuatilia akaunti zao za binafsi na za kibiashara kwa wakati mmoja.
Huduma zipatikanazo kwenye programu hii ni: huduma za kuhamisha fedha, huduma za hundi, maombi ya mkopo wa papo hapo, malipo ya bili mbalimbali, huduma za utoaji fedha kwenye ATM bila kadi, kuongeza muda wa maongezi, usajili binafsi wa mobile banking na huduma za e-chama pamoja na nyingine nyingi.
Zaidi ya hayo, SWAHIBA Mobile APP inaweza kutumiwa na Mtanzania yoyote hata ambae si mteja wa BANK OF AFRICA. Hii ni kupitia huduma mbalimbali zinazopatikana kabla ya kuingia kwenye program yaani “without Log in services”. huduma hizi ni kama vile maelezo kuhusu Huduma mbalimbali zitolewazo na BANK OF AFRICA, Maombi ya Mikopo, maelekezo kuhusu yalipo Matawi ya BANK OF AFRICA na ATMs, pamoja na viwango vya ubadilishaji fedha za kigeni.
Mr. Ammishaddai Owusu-Amoah, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa BANK OF AFRICA - TANZANIA alisema Benki yake inajivunia kuanzisha programu hii mpya ya benki kiganjani katika wakati huu muhimu ambapo benki hiyo inaadhimisha miaka 10 ya biashara katika nchi ya Tanzania. "Uzinduzi wa SWAHIBA Mobile App ni namna ya kipekee ya kuwasilisha shukrani zetu kwa wateja, jamii, washirika, wamiliki na wadau wote, walio tupa ushirikiano wa kutosha katika kipindi cha miaka 10 ya kazi nchini ".
"Huduma hii pia inakuja kutia msistizo wa ahadi yetu ya kuweka mapendekezo ya wateja wetu kwanza na kuwaongezea uzoefu wa kidigitli Zaidi katika ukuwaji wa sayansi na technologia. Mkurugenzi aliendelea kueleza “Pia inathibitisha uamuzi wa benki wa kujenga uwepo wake wa kidigitali na kukidhi mahitaji ya haraka ya wateja wetu "
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Hivyo makala BANK OF AFRICA – TANZANIA yazindua program mpya ya kibenki ya “SWAHIBA MOBILE APP”
yaani makala yote BANK OF AFRICA – TANZANIA yazindua program mpya ya kibenki ya “SWAHIBA MOBILE APP” Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BANK OF AFRICA – TANZANIA yazindua program mpya ya kibenki ya “SWAHIBA MOBILE APP” mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/bank-of-africa-tanzania-yazindua.html
0 Response to "BANK OF AFRICA – TANZANIA yazindua program mpya ya kibenki ya “SWAHIBA MOBILE APP”"
Post a Comment