Askofu Gadi: Watanzani tunzeni mazingira

Askofu Gadi: Watanzani tunzeni mazingira - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Askofu Gadi: Watanzani tunzeni mazingira, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Askofu Gadi: Watanzani tunzeni mazingira
kiungo : Askofu Gadi: Watanzani tunzeni mazingira

soma pia


Askofu Gadi: Watanzani tunzeni mazingira


Na. Neema Mathias-MAELEZO.

Askofu wa kanisa la Good News For All, Dkt. Charles Gadi ametoa wito kwa wananchi na serikali kuyatunza mazingira na uoto wa asili ili kuchangia uwepo wa hali nzuri ya hewa.

Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam na Askofu Gadi, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo aliongoza maombi maalum kwa lengo la kuombea tahadhari iliyotolewa na Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa juu ya uwezekano wa kutokea kwa upungufu mkubwa wa mvua za vuli katika mikoa mingi hapa nchini.

Askofu Gadi amesema kuwa wananchi wote wanapaswa kulinda mazingira ikiwemo kupiga vita ukataji ovyo wa miti na badala yake wapande miti kwa bidii ili kuilinda mazingira kutokana na uharibifu unaosababisha ukame unaotokana na ukosefu wa mvua.

Aidha askofu huyo amesema kuwa wao kama viongozi wa dini wanakubaliana na utabiri wa kisayansi uliotolewa ambao mara nyingi umekuwa ukifanikiwa, lakini haitokuwa sawa kusubiri hadi hali hiyo ya ukame itakapotokea wakati Mungu amewapa Imani na mamlaka ya kuomba dhidi ya majanga kama hayo.

“Good News for All kwa kushirikiana na madhehebu mbalimbali tumekuwa tukiendesha mikutano ya kuiombea nchi dhidi ya ukame tangu mwaka 2006 ambapo ni zaidi ya miaka 11 sasa tunamshukuru na Mungu amekuwa akijibu maombi yetu,” alisema Askofu Gadi.
Mwenyekiti wa Kanisa la Good News For All Ministry Askofu Dkt. Charles Gadi (katikati) akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati akifanya maombi maalumu ya kuombe mvua mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Katibu wa kanisa hilo Mchungaji Palemo Massawe na kushoto ni Mchungaji wa kanisa hili Andrew Thomas.
Mwenyekiti wa Kanisa la Good News For All Ministry Askofu Dkt. Charles Gadi (wa pili toka kulia) pamoja na wachungaji wa kanisa hilo wakifanya maombi maalumu ya kuombe mvua mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kanisa la Good News For All Ministry Askofu Dkt. Charles Gadi wakati akifanya maombi maalumu ya kuombe mvua mapema hii leo jijini Dar es Salaam.Picha na Eliphace Marwa – Maelezo.



Hivyo makala Askofu Gadi: Watanzani tunzeni mazingira

yaani makala yote Askofu Gadi: Watanzani tunzeni mazingira Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Askofu Gadi: Watanzani tunzeni mazingira mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/askofu-gadi-watanzani-tunzeni-mazingira.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Askofu Gadi: Watanzani tunzeni mazingira"

Post a Comment