title : WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AAGIZA WAENDESHA BODABODA WOTE KUNUNUA KOFIA NGUMU NDANI YA MWEZI MMOJA
kiungo : WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AAGIZA WAENDESHA BODABODA WOTE KUNUNUA KOFIA NGUMU NDANI YA MWEZI MMOJA
WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AAGIZA WAENDESHA BODABODA WOTE KUNUNUA KOFIA NGUMU NDANI YA MWEZI MMOJA
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mheshimiwa Mwigulu Nchemba ameagiza waendesha bodaboda wote nchini kuhakikisha kuwa wanakuwa na kofia ngumu ‘Helmet’ ndani ya mwezi mmoja baada ya hapo hatua kali zitachukuliwa.
Mheshimiwa Nchemba ametoa agizo hilo jana Agosti 26,2017 mjini Shinyanga wakati akizungumza na waendesha bodaboda na baiskeli 'daladala' zaidi ya 300 wanaofanya shughuli zao katika manispaa ya Shinyanga.
Alisema kosa la kutovaa kofia ngumu litawahusu wamiliki wa bodaboda,waendesha bodaboda pamoja na abiria ambao kwa pamoja watawajibika kila mmoja kwa nafasi yake.
“Hili litafsiriwe vizuri kila eneo katika nchi yetu,kwanza kabisa kama mmiliki hajaweka kofia mbili,bodaboda ikikutwa haina kofia mbili,tatizo lile linaenda kwa mmiliki,pili kama mwendesha bodaboda amepewa kofia mbili halafu akaamua kuziacha huyo ana kosa”,alieleza.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mheshimiwa Mwigulu Nchemba akizungumza na waendesha bodaboda na baiskeli 'daladala' jana mjini Shinyanga.Kulia ni Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Simon Haule.Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack.
Mkazi wa Shinyanga Mjini akieleza shida yake kwa Waziri wa Mambo ya Ndani,Mheshimiwa Mwigulu Nchemba baada ya kikao kufungwa.Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mheshimiwa Josephine Matiro akizungumza wakati wa kufunga kikao hicho.
Hivyo makala WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AAGIZA WAENDESHA BODABODA WOTE KUNUNUA KOFIA NGUMU NDANI YA MWEZI MMOJA
yaani makala yote WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AAGIZA WAENDESHA BODABODA WOTE KUNUNUA KOFIA NGUMU NDANI YA MWEZI MMOJA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AAGIZA WAENDESHA BODABODA WOTE KUNUNUA KOFIA NGUMU NDANI YA MWEZI MMOJA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/waziri-mwigulu-nchemba-aagiza-waendesha_27.html
0 Response to "WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AAGIZA WAENDESHA BODABODA WOTE KUNUNUA KOFIA NGUMU NDANI YA MWEZI MMOJA"
Post a Comment