WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA CHA KUZALISHA SUKARI NCHINI CUBA

WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA CHA KUZALISHA SUKARI NCHINI CUBA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA CHA KUZALISHA SUKARI NCHINI CUBA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA CHA KUZALISHA SUKARI NCHINI CUBA
kiungo : WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA CHA KUZALISHA SUKARI NCHINI CUBA

soma pia


WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA CHA KUZALISHA SUKARI NCHINI CUBA

Mwambawahabari


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Shirika la Viwanda vya Sukari nchini Cuba, Bw. Francisco Lled, ambaye amekubali kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuongeza uzalishaji wa sukari nchini.


Shirika la Sukari la nchini Cuba linauwezo wa kuzalisha tani milioni nne za sukati kwa mwaka huku mahitaji ya ndani ni tani 700,000, ambapo kiasi kinachobaki huuzwa nje ya nchi. Kwa sasa shirika hilo linazalisha tani milioni mbili tu katika viwanda vyake 56.


Waziri Mkuu alikutana na Bw. Lled jana (Alhamisi, Agosti 24, 2017), wakati alipofanya ziara katika kiwanda cha kuzalisha sukari cha UGB Central Azucarero 30 de Noviembre katika mji wa San Nicola’s de Bari ambacho ni kati ya viwanda 27 vya shirika hilo linalomilikiwa na Serikali ya Cuba kwa asilimia 100.

Katika mazungumzo yao Waziri Mkuu alimshawishi Bw. Lled kuja nchini kwa ajili ya kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya kuzalisha sukari. Alisema kwa sasa Tanzania kuna viwanda vikubwa vitano vya sukari ambavyo uzalishaji wake hautoshelezi mahitaji ya ndani.

Waziri Mkuu alivitaja viwanda hivyo ambavyo ni Mtibwa na Kilombero (Morogoro), Mahonda (Zanzibar), TPC (Kilimanjaro) na Kagera ambavyo vyote vinazalisha jumla ya tani 320,000 za sukari kwa mwaka huku mahitaji yakiwa ni zaidi ya tani 400,000.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi inatarajia kujenga viwanda vitatu vya kuzalisha sukari, ambavyo vitazalisha sukari itakayotosheleza mahitaji na ndani ya nchi na kiasi kitakachosalia kitauzwa nje.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipata maelezo ya ukarabati wa kiwanda cha Sukari cha UGB  kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari nchini Cuba Bwana Francisco Martin, jana August 24/2017 kiwanda hicho kipo katika Mji wa San Nicola's de Bari nchini Cuba

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia shehena ya sukari iliyozalishwa katika kiwanda cha UGB Central Azucarero 30 Noviembre wakati alipotembelea kiwanda hicho jana August 24/2017 kilichopo katika mji wa San Nicola's de Bari nchini Cuba.


Hivyo makala WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA CHA KUZALISHA SUKARI NCHINI CUBA

yaani makala yote WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA CHA KUZALISHA SUKARI NCHINI CUBA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA CHA KUZALISHA SUKARI NCHINI CUBA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/waziri-mkuu-atembelea-kiwanda-cha_25.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA CHA KUZALISHA SUKARI NCHINI CUBA"

Post a Comment